SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Faida 3 Za Elegant / Classy Style
Mitindo

Faida 3 Za Elegant / Classy Style 

Kwa namna ambavyo Dunia inaenda sasa watu wengi wanawake kwa wanaume hawajali namna ambavyo wanaonekana, unaweza kusema mbona sasa hivi ndio watu wanajali mionekano tunaweza kusema ni watu wachache sana wanaangalia wanachovaa, wengi tunavaa tu ilimradi tuvae, unaweza kukuta mtu amevaa nguo za gym akiwa anafanya shopping au matembezini, unaweza kukutana na mtu kavaa viatu vya kutembelea ndani nje, yes tunavaa lakini hatujali namna ambavyo tunaonekana au kama hilo vazi linafaa sehemu uendayo.

Kwasababu hizi ukivaa vyema basi una stand out na kuwa wa tofauti kama ambavyo kuna msemo unasema “in the world full of Kardashian be the Beyonce”, Je kunafaida gani za ku-stand out na kuwa classy / elegant?

  • Unaongeza Kujiamini

Unapovaa vyema kutokana na mazingira, unachoenda kufanya basi unakuwa unajiamini zaidi na kuweza kufikia malengo yako na zaidi kuliko ukiwa umevaa hovyo utaanza kujishtukia na kupunguza kujiamini kwako.

  • Kupata Fursa Nyingi Zaidi

Kwasababu unajiamini basi wengine pia watakuamini na kukupa nafasi zile ambazo nyingine hata hukuzitegemea, unaweza kuona haya hasa pale kinapotokea kitu kwa mtu ambae anapendeza watu wanasema mbona hafananii na muonekano wake? Hii ni kwamba watu wanaamini katika mionekano zaidi.

Faida Za Kuvaa Vizuri 

  • Kuheshimiwa / Kutendewa Vizuri

Kama tulivyosema hapo juu unapovaa vyema unaaminika zaidi na watu wata ku-treat vizuri kutokana tu na namna ambavyo umejionyesha kwao, hata barabarani wengi wakikuta umevaa suit au umependeza watakuita boss wakati ukiwa hovyo hakuna ambae atajisumbua na wewe.

Well jaribu kubadilika na kupendeza kisha utuambie ni namna gani huko kwenye matembezi yako wamekupokea.																			

Related posts