SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fashion Resolution Kwa Ajili Ya Mwaka 2020
Mitindo

Fashion Resolution Kwa Ajili Ya Mwaka 2020 

Mwaka umekaribia kuisha, tuna masaa kadhaa kabla hatujaanza mwaka mpya, sisi huwa tunapenda kuwakumbusha malengo ya kujiwekea ifikapo mwaka mwingine hasa katika swala zima la mitindo. Hii inaweza kukusaidia ku-improve muonekano wako lakini pia kukusaidia katika uhifadhi ya pesa.

Mwaka jana tuliandika malengo kumi, mwaka huu tunahaya malengo machache tu.

Malengo Kumi (10) Ya Kujiwekea Kwa Ajili Ya Kuanza Mwaka Mpya Kwa Umaridadi

 • Jifunze kukubali mwili wako

Kama kunakitu ambacho tumejifunza kutokana na blogging ni kwamba watu wengi hawajiamini na miili yao. Pale tunapoandikia kuhusu mavazi fulani wengi husema hio inawapenda wenye aina fulani ya miili, au mimi nina tumbo kubwa hakinifai, tungependa mwaka huu wenye self doubt na miili yenu mjifunze kuipenda, hii itakupa confidence lakini pia kukufanya uvae mavazi yanayoendana na wewe.

Tatizo Si Mwili Wako Bali Ni Fikra Zako Juu Ya Mwili Wako

 • Huitaji Mavazi Mapya.

Yes usipoteze muda wako kwa kununua mavazi mapya kwa mara, unachotakiwa kufanya ni kuwa m’bunifu kwa yale ambayo uliyokuwa nayo . Revamp, Recycle kile ulichonacho na create new outfit.

 • Invest In Real Statement Pieces

Ukiwa na vitu viwili au vitatu ambavyo vina quality nzuri na unaweza kuvirudia mara nyingi ni kitu kizuri, kila siku unaonekana umevaa kitu quality na fashionable. Achana na kununua vitu ambavyo vina quality mbaya na vingi kuwa na vitu vichache vinavyo make statement na quality yake ni nzuri.

 • Don’t Be Boring

Kiatu,shirt na suruali hiyo ni boring outfit jaribu kuongezea vitu vingine kama pochi, hereni, saa, koti, mkanda, mkufu n.k & stand out.

Ni matumaini yetu 2020 utakuwa fashionable year kwetu sote.

Related posts

2 Comments

 1. useful site

  … [Trackback]

  […] Here you will find 22520 more Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-resolution-kwa-ajili-ya-mwaka-2020/ […]

 2. twittervideodownloader

  … [Trackback]

  […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-resolution-kwa-ajili-ya-mwaka-2020/ […]

Comments are closed.