SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fashion Tips For Plus Size Women
Dondoo

Fashion Tips For Plus Size Women 

Miaka ya nyuma watu wenye miile minene walikuwa wanapata sana shida kujua wavae nini na wavaeje, ilikuwa shida zaidi kwa maana nguo nyingi zilikuwa zina buniwa kwa ajili ya watu wenye miili midogo lakini kwa sasa dunia imebadilika na wao wanapata mavazi yao na hata kushirikishwa katika runways, Plus size & slaying.

Leo tumeona tuwaletee fashion tips tatu ambazo zinaweza kukusaidia kama una mwili mkubwa (mnene)

Highlight zile feature zako nzuri – watu wengi wenge miili mikubwa huwa wanakosea kwa kuvaa vitu kama ambavyo wanavyo vaa watu wenye miili midogo mf: mtu mwele mwili mdogo anaweza kuvaa gauni na belt akafungia belt tumboni, yes anaweza sababu tumbo lake ni dogo lakini kam wewe ni mnene na unatumbo kubwa hupashwi kuvalia mkanda hapo, valia mkanda juu ya kiuno au chini kidogo ya matiti hii itasaidia sio tu kuficha tumbo lako bali pia kuonyesha shape yako vizuri.

Usione aibu kuonyesha mwili wako – hili ni tatizo ambalo wengi wanalo utakuta mtu ambae ni plus size anavaa nguo kubwa ndefu,ukimuuliza kwanini atasema labda nina mikono minene au nina miguu minene bila kujua kama anaweza kuonyesha hizo sehemu na akapendeza tu bila ya tatizo.

Cheza na pattern – wengi huwa tunavaa nguo nyeusi (hii inasemekana ina saidia kukufanya uonekane mwembamba) achana na hio dhana jua kucheza na pattern na utashangaa jinsi ambavyo unaweza kuvaa rangi lakini pia ukapendeza na huo huo mwili wako.

Mwisho jipenda na kuwa na confidence kwamba your beautiful the way you are. kusoma tips nyingine unaweza ku click hapa.

Related posts

Leave a Reply