Wakati tuna “Chit Chat” katika social networks zetu, baadhi ya afromates walitoa request za nini tuandikie na tips gani tuwape. Hili swali lilionekana kujirudia mara nyingi, wengi waliulizia fashion tips kwa mtu mwenye matege.
Matege ni ugonjwa unaompata mtu au mnyama mwenye ukosefu wa vitamini D mwilini, hasa miezi ya kwanza ya maisha yake.
Wengi ambao wanatatizo hili hukosa amani ya kuvaa baadhi ya mavazi kama skin jeans, nguo fupi na vingine vingi kwa kuhofia miguu yao kuonekana imepinda.
Ambacho tungependa kusema cha kwanza ni kwamba jipende namna ulivyo, ukijipenda na kuwa na confidence basi hutoweza kufikiria mara mbili kuhusu miguu yako, cha kwanza kabisa mara nyingi watu huwa hawa-notice miguu yako bali ni ile hali ambayo tumejiwekea kichwani nina matege, au nikivaa kitu fulani sipendezi.
Tatizo Si Mwili Wako Bali Ni Fikra Zako Juu Ya Mwili Wako
- Draw Attention Away From Your Legs
Kama bado unahisi kwamba huna ujasiri wa kutosha kuvaa mavazi yanayo onyesha miguu yako, basi chagua kutoa attention maeneo hayo. Vaa nguo ndefu iwe skirts au magauni chagua ambayo ni full length.
- Flared Jeans, Mom Jeans au Bwanga
Kama unaona skinny jeans zinachora miguu yako basi vyema ukavaa flared jeans, mom jeans au hata mabwanga ili kuweza kuficha au kuondoa attention katika miguu yako.
- Cropped suruali

Lakini kama umpenzi wa skin jeans basi njia mojawapo ya kufanya matege yako yasionekane sana ni kukunja suruali yako au kununua suruali ambayo ni cropped hii inasaidia kutokuonyesha matege yako kwa kiasi fulani.
- Mid Length Dresses & Skirts

Kama ambavyo tuliona katika suruali basi kwenye skirt na magauni pia ni vyema kuvaa ambazo urefu wake unaishia katikati ya matege yako.
- Chaguo Sahihi La Viatu

Kama unapenda kuvaa nguo fupi basi hakikisha unafanya chaguo sahihi katika uchaguzi wa viatu, unapo vaa nguo fupi na flat sandals hii inafanya miguu yako ichoreke zaidi lakini kama utavaa ankle boots, over the knees boots ambazo hazibani miguu, wedges, low heels zinaweza kusaidia kupunguza uonekanaji wa matege yako.
Related posts
7 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-tips-kwa-watu-wenye-matege/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-tips-kwa-watu-wenye-matege/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-tips-kwa-watu-wenye-matege/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-tips-kwa-watu-wenye-matege/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-tips-kwa-watu-wenye-matege/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-tips-kwa-watu-wenye-matege/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-tips-kwa-watu-wenye-matege/ […]