“Sina Cha Kuvaa” hili neno linatumika karibu na kila mwanamke ifikapo asubuhi anataka kwenda kazini,wakati wa mitoko nakadhalika, lakini cha kushagaza makabati huwa yamejaa nguo mbali mbali lakini bado huwa tunakosa cha kuvaa (confusing right?). Wengi huwa tunanua nguo nyingi kila siku kwa kudhani tu hatuna nguo za kutosha maana kila mara tunakosa cha kuvaa, Calm down nguo unazo za kutosha unahitaji kujua tips hizi chache za nini cha kufanya unapo hisi huna cha kuvaa.
- Vaa nguo nyeusi full – wanasema “when in doupt wear black” na “you never go wrong with black” lakini pia neutral color ni angi nzuri pale unapo hisi huna cha kuvaa rangi kama nyeusi, beige,nyeupe ni chaguo zuri linapo kuja swala la kukosa cha kuvaa
- Basic white t-shirt na flat shoes – ni chaguo lingine zuri linalo weza kukusaidia pale unapo kwama kujua uvae nini kitu kizuri kuhusu white tee na flat shoes unaweza kustyle na chochote suruali,skirt au kaptura
- Gauni X Sneakers – hili ni chaguo zuri pale unapo kosa cha kuvaa na hujisikii ku match na kumix nguo kimbilia gauni na sneakers kama ni kazini unaweza kutupia na blazer.
- White Shirt & Heels – always does the trick hapa pia unaweza kuvalia skirt, suruali au kaptura ni rahisi lakini pia chic
- Oversized Denim Jacket – pale unapo hisi mtoko wako ume bore ongezea denim jacket kwa juu
- Colorful Coats – hii itakusaidia kuupa mtoko wako muonekano mpya hasa kama umevaa mavazi ya rangi zilizo fifia well when on a bad outfit days pop it with some color.
- Accessorize – chukua attention ya mavazi na weka katika urembo, vaa hereni au mikufu inayo shout itakayo wafanya watu waache ku-concetrate na mavazi yako na kuwa wana concentrate na accessory zako
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…