SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fashion Trend Za Kuongeza Katika Kabati Lako Kabla Ya 2020 Haijaisha
PARIS, FRANCE - FEBRUARY 26: A guest is seen wearing mini Jacquemus bag outside Marques Almeida during Paris Fashion Week Womenswear Fall/Winter 2019/2020 on February 26, 2019 in Paris, France. (Photo by Christian Vierig/Getty Images)
Mitindo

Fashion Trend Za Kuongeza Katika Kabati Lako Kabla Ya 2020 Haijaisha 

2019 ulikuwa mwaka mzuri kwa fashion na trend nyingi za mwaka huu zilianza nwaka jana. Elegance is about being classy, japokuwa tunapenda kuwa na vitu classy katika kabati. Ni vyema kuongeza piece kadhaa zinazoendana na wakati ili kuchangamsha muonekano. Kumekuwa na trends nyingi zilizotawala mwaka huu. Kwa bahati mbaya 2020 imepoa kidogo kwasababu ya limit ya movement lakini we can still slay ofisini, nyumbani na sehemu chache tunazoenda. Hizi ni trends zitakazoboresha muonekano wako.

  • Pochi Ndogo

Pochi ndogo zimekuja kwa kasi sana. Zinamuonekano wa kipekee. I think they are so cute na zimekaa kidada zaidi tofauti na pochi kubwa. Sasa hivi kuna hadi pochi ndogo sana inatosha kuweka pesa tu. Hii trend imenikumbusha kipindi pochi kubwa sana zilikuwa trend, ukiweka daftari humo basi unajiona wewe ni wewe. Pochi ndogo ni rahisi kubeba kwa kuning’iniza mkononi. And kuna something about them hufanya mtu aonekane delicate. 

  • Mismatch

This year we are going poker. Kama ulishawahi kuona joker basi unafahamu huwa limevaa nguo ina rangi moja upande mmoja na nyingine upande mwingine. Hii trend imeibuka katika mavazi mbalimbali mwaka huu. Kwanzia kwenye nguo, viatu hadi handbag. Mavazi yenye design moja upande mmoja na nyingine yamezidi kutrend. Utofauti wa design unaweza kuwa katika rangi, shape au details nyingine.If you are bold and daring, hii ni trend nzuri ya kuongeza katika kabati yako. 

  • Puffy Sleeves
This image has an empty alt attribute; its file name is SGs3M5WZUQV8PGGj8o45GWpvUIJ_rM6N4lQ0fnYU75HR5addIT1rhDKlgv72dA90IbDoWNmlw1B2yHepdTmFm53UZCeFBo-Ru_XLS77VGsLMxupECcNgjHW5vSXVbJUfLTC7E9uHDUKg4gm_vA

Statement tops ni nzuri hatari, hazihitaji kusindikizwa na accessories nyingi. Zenyewe tu zinatosha kubeba muonekano wote. Top yenyewe kama yenyewe inaonesha uko stylish. Top zenye mikono iliyojaa (puffy) ni moja ya statement tops. Top hizi hubeba sana muonekano. Good thing top hizi huja kwa mitindo mbalimbali so you can chose puffy sleeves zinazoendana na taste yako. Wengine hupenda mikono iliyojaa kiasi wakati wengine wakipenda zaidi mikono iliyojaa kidogo tu.

  • Sketi Ndefu Za Jeans

Sketi za jeans zimekuwepo miaka nenda rudi. Mwaka huu in particular sketi ndefu za jeans zimetrend zaidi. Sketi zinazovuka goti, either mpaka katikati ya miguu au zinazofika chini kabisa.Sketi za jeans huwa na mpasuo katikati kwa mbele au nyuma na nyingine huwa plain tu. Kuna njia nyingi ya kustyle sketi hizi lakini kama suruali, sketi hizi kuendana na nguo nyingi. Sketi ya jeans ya penseli (pencil skirt) hukaa kike zaidi.

  • Long Blazer
This image has an empty alt attribute; its file name is WTlgJvkKXBPWPBDiXzSJo1V5GwLcC50WBWUZy2GnOTKxwSTaKlK2Mr7xEXe-bIhptihauTNxdm5cZ70zzz5nZndwJG6xKMID7EeM_V2BLQuwStwRjv5FG4RzyAj-UdYki7s6aX9h8M0apIsY2A

Koti ni sehemu kubwa ya uvaaji kwa wanawake, hali ya hewa inaporuhusu blazers huwa vazi pendwa. Blazer zilizozoeleka zaidi ni zile fupi zinazoishia kiunoni. Blazer ndefu zimezidi kutrend mwaka huu, blazer hizi hufunika mpaka kwenye hips. Blazer hizi ziko stylish sana na huboresha sana muonekano hususani zinapovaliwa na nguo sahihi.

  • Polka Dots

Polka dots zilianza kutrend mwaka 2019 na zinazidi kutrend. Polka dots huongeza details katika vazi. Zinafanya hata nguo simple sana isiboe. Polka dots zilizozoeleka zaidi ni nyeusi katika nguo nyeupe na nyeupe katika nguo nyeusi. Good news ni, polka dots zinaweza kuwa za rangi pia so sio lazima ustick na black and white. Kama sio mpenzi sana wa prints, unaweza kuanza na polka dots badala ya kuvaa nguo zenye prints kubwa.

  • Square Toe Shoes

Ni vizuri kuwa na kitu tofauti na fresh katika  kabati lako. Viatu unique hufanya nguo ipop zaidi. So ukivaa viatu unique na nguo simple sana bado utaonekana kama umeweka effort katika uvaaji wako.

To be honest baadhi ya hivi viatu huwa na muonekano wa ajabu. Tena kama hauujulii mguu wako unaweza kuambulia the wrong shoes. Hivi viatu viko tricky so be careful wakati wa kuchagua na kama vimefunika sometimes they look kama vya kiume. 

Unapochagua hivi viatu jaribu kwanza, hakikisha vidole vinakaa vizuri kama kiatu ni cha wazi, hususani kama kiatu ni kirefu. Hakikisha mikanda ya kiatu inabana vizuri mguu wako na kukupa uhuru unapotembea.

Kwa kiatu flat jitahidi kuchagua kiatu ambacho hakifuniki sehemu kubwa sana ya mguu. Kama kikifunika sehemu kubwa then valia nguo isiyofunika miguu.

  • Chuichui Na Gamba La Nyoka

Chuichui hupendeza sana, I really love it. Sidhani kama chuichui humchukiza mtu. It is a perfect blend of browns and black. Chuichui hupop zaidi ikivaliwa na solid color badala ya print nyingine. Namaanisha vaa chichui na Rangi moja tu ili focus iwe kwenye chuichui zaidi. Chuichui hupendeza na nyeupe, nyeusi, brown, kaki. Chuichui ni moja ya print rahisi zaidi kuvaa hata kwa wasiopenda prints. Chuichui imezidi kutrend mwaka huu, ni trend hutajuta kuongeza katika mavazi yako.

Unlike chuichui, gamba la nyoka huja katika rangi nyingi tofauti. Japokiwa chui inazidi kutrend mwaka huu, tunafahamu imekuwepo kwa muda sasa. Gamba la nyoka kwa upande mwingine sio pattern ambayo imevalika sana. Kama unataka a completely fresh look basi vaa gamba la nyoka katika rangi unayopendezwa nayo zaidi.

  • Mavazi Ya Kufuma ( Knit Wear )
This image has an empty alt attribute; its file name is ZVWxxP-wqoHuEhJaD1CPN80IY6IlGS6w4STIu_t6dQJV67u2IepVI57SvUV6WLND7hy_gSLAHiITxKBWlXvkQGt0k2LF3Cy14PjHxg0NIJKv_-19XEqBHPbT1QYIqaqDOrmWYhjf0TaG3Dy19g

Kama unapenda kushop au kuwindow shop, I’m sure umekutana na nguo za kufuma. Zimekaa kama sweta ila katika mavazi mbali na sweta kama gauni, two pieces, tops na sketi. Uzuri ni kwamba baadhi ya nguo hizi huwa nyepesi, hazifumwi kama masweta hivyo usipate hofu. Nguo zilizofumwa huwa na details bila hata kuongezewa kitu kwasababu ya kitambaa chake na movement za nyuzi. Kuna accessories pia za kufuma kama mikoba na scarf.

  • Nguo Za Marinda
This image has an empty alt attribute; its file name is 1oFrpDSon0WYBR-iE2jbA4iDHp0zTgp1SARuH_MGqucDEoaf_QBVbSYjeP4UULSPh8OkYR-OfvsmGspB0SG8-bEhFzAypI02-8YkIENT9cmUP0XagMDEmZZeMVQ20NC6iZgdIiQ5BnfjJSe7Mw

Marinda yamekuwepo kwa muda mrefu, tumezoea zaidi kuona marinda kwenye sketi. Marinda yamezidi kutawala katika mavazi mbalimbali na kwa sasa marinda yamekuwa kama urembo katika tops, sketi, koti na hata suruali. Marinda yanaupgrade muonekano, yatafanya uonekane wa kisasa zaidi. Pia ni namna nzuri ya kuchangamsha mavazi ya kiofisi yanayoboa.

  • Lulu (Pearls )

Lulu zimezagaa kwelikweli mwaka huu, lulu bandia actually. Lulu halisi huwa na gharama sana kwasababu hazipatikani kwa urahisi. Lulu zimekuwa pambo la kila kitu; nywele, hereni, cheni, mikono ya mikoba, mikanda ya viatu n.k. Lulu huvutia na zimekaa kike sana hivyo humpa mvaaji muonekano wa kike but classy. Lulu hazipaishwi sana kama chuma, dhahabu au alhamis lakini ni accessory nzuri mno inayofanya mwanamke aonekane delicate.

Pamoja na Lulu kukaa kike sana, baadhi ya wanaume wamekuwa daring enough kuzivaa na kuzistyle katika mavazi ya kiume. And to be honest zimekaa fresh tu kwa baadhi yao.

Hizi ni baadhi tu ya trends. There is more. I hope you will have wakati unaongeza trend hizi katika mavazi yako. Be bold na fanya majaribio ya kustyle katika namna mbalimbali. Until next article, lots of love from elegancebyree.

Related posts

5 Comments

  1. Plantation Shutters

    … [Trackback]

    […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-trend-za-kuongeza-katika-kabati-lako-kabla-ya-2020-haijaisha/ […]

  2. 늑대닷컴

    … [Trackback]

    […] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-trend-za-kuongeza-katika-kabati-lako-kabla-ya-2020-haijaisha/ […]

  3. 토렌트

    … [Trackback]

    […] Here you will find 96407 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-trend-za-kuongeza-katika-kabati-lako-kabla-ya-2020-haijaisha/ […]

  4. บ้านมือสอง

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-trend-za-kuongeza-katika-kabati-lako-kabla-ya-2020-haijaisha/ […]

  5. ufabtb

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashion-trend-za-kuongeza-katika-kabati-lako-kabla-ya-2020-haijaisha/ […]

Comments are closed.