SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

7 Things To Do While You Are Stuck At Home During Quarantine
AfroTipAndTricks

7 Things To Do While You Are Stuck At Home During Quarantine 

Wakati tukiwa tumezoea ikifika weekend tunatoka kwenda kwenye manunuzi, kufurahi na kujumuika na ndugu na marafiki kufanya usafi wa nywele zetu na kucha. Kwa sasa haiwezekani kutokana na uganjwa hatari wa Corona. Tumeshauriwa kukaa mbali na mikusanyiko na kama huna cha maana mtaani ni bora ukakaa tu nyumbani kwako.

Unaweza kujiuliza corona ni nini “Corona ni – ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu. Kwa binadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji.  Maradhi yaliyowahi kusababisha madhara makubwa kutokana na virusi vya Corona ni pamoja na MERS na SARS yaliyozuka mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kirusi cha Corona kilichogundulika hivi karibuni kinasababisha ugonjwa unaofahamika kama COVID-19.

COVID-19 ni nini?

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

Baada ya kujua kuhusu Corona na COVID-19 Utajiuliza ni namna gani unaweza kujikinga. Moja kati ya njia kadhaa wa kadhaa za kujikinga na ugonjwa huu ni pamoja na kujiepusha na mikusanyiko ya watu na kukaa nyumbani. Well kwa wale tuliozoea parte after parte hii ni ngumu kidogo basi ufanye nini ukiwa nyumbani peke yako?

 • Safisha kabati lako

Tumia muda huu kusafisha kabati lako la mavazi na panga vyema mavazi yako, toa yale machafu yafuliwe, yaliyo chanika yaweke pembeni kwa ajili ya kupelekwa kwa fundi, ambayo hujayavaa siku nyingi yatenge pembeni kwa ajili ya kuyagawa au kuuza lakini pia tumia muda huu kujua nini kinafaa kubaki kwenye kabati na kipiunahisi kimepitwa na wakati na huwezi kukivaa tena.

 • Mix and match mavazi yako ili kupata ideas mpya za mavazi ambapo wakati ulikuwa huna muda hukuweza kufanya
 • Dress up na angalia nini kinakupendeza
 • chukua muda wako kulisoma kabati lako na kujua style ya mavazi unayoyapendelea.

Jinsi Unavyoweza Kubadilisha Wardrobe Yako Kutokana Na Umri Na Mazingira

 • Safisha kabati la viatu

Kama katika kabati la nguo twende pia kwenye viatu, hapa huwa tunajisahau sana unaweza kukuta viatu havijavaliwa miaka, vinavumbi, vingine vimeharibika lakini pia vingine vimeshakuwa vidogo. Toa ambavyo unaona vinafaa kuendelea kuwepo uvishafishe na kuvipanga upya na vile ambavyo unaona havifai tena unaweza kuvigawa au kuuza au hata kuvitupa.

 • Safisha dressing table

Yes toa makopo ambayo yameisha dawa, perfume, body spray na uyatupe, angalia nini kime expire nacho ukitupe, chukua muda wako kuangalia product unazozituma na zipange na vyema na ambazo huzitumii uzipunguze katika dressing table yako.

Namna ya kupanga dressing table

 • Fumua / Osha nywele zako

Sio lazima kwenda salon unaweza kutumia hii kujifanyia self care mwenyewe kwa kufumua, kuosha au kama una product nyumbani kujifanyia steaming mwenyewe.

VITU 7 KUTOKA JIKONI VINAVYO WEZA KUSAIDIA UKUAJI WA NYWELE ZAKO

Makosa Unayofanya Wakati Wa Kuosha Nywele Zako

 • Safisha / kata kucha

Kitu kingine ambacho huitaji kutoka nje kwenda kukifanya ni kusafisha kucha zako, yes tumezoea kwenda kufanya manicure na pedicure lakini tunaweza kujifanyia hivi wenyewe hata tukiwa nyumbani.

Namna Ya Kuondoa Kucha Za Kubandika (fake nails) Mwenyewe

NG’ARISHA KUCHA ZAKO BILA KUTUMIA RANGI YA KUCHA

 • Skin Care

Unaweza kujijali mwenyewe kwa kufanya skin care kwa kutumia vitu ulivyo navyo, kama manjano, liwa, mtindi etc etc tumia muda huu ambao upo nyumbani kuiweka ngozi yako vizuri kabisa.

Njia Rahisi za Kutunza Ngozi Yako Ya Uso Katika Weekend

 • Selfcare

Unaweza kutumia muda huu kujijali wewe mwenywe, lala vizuri, fanya mazoezi, fanya yoga, soma vitabu, jaribu kuangalia na kupangilia milo yako na mengine mengi.

Ni matumaini yetu tumekusaidia na umepata wazo la nini ufanye wakati huu ambapo upo nyumbani.

Related posts

3 Comments

 1. wapjig.com

  … [Trackback]

  […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashionably-things-you-can-do-while-your-stuck-in-quarantine/ […]

 2. 2 hour weed delivery toronto

  … [Trackback]

  […] There you will find 98324 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashionably-things-you-can-do-while-your-stuck-in-quarantine/ […]

 3. springfield farms carts

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/fashionably-things-you-can-do-while-your-stuck-in-quarantine/ […]

Comments are closed.