SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Flat Sandals Outfit Ideas From Julitha Kabete
Mitindo

Flat Sandals Outfit Ideas From Julitha Kabete 

Viatu virefu sio ufunguo wa vazi kuonekana classy na elegant,inawezekana ukavaa viatu virefu vizuri lakini bado ukaonekana messy, inawezekana ukawa umekosea kwenye mavazi au accessories zako, cha muhimu katika kuchagua mavazi na viatu ni kuangalia kipi kinaendana na kipi.

Kuna aina viatu ambavyo hutoa vibe ya casual look ambapo wengi tunaamini viatu kama sneakers, sandals, flats zinafanya muonekano uonekane casual na sio elegant, lakini kumbe unaweza kuvaa aina hio ya viatu na bado muonekano wako ukawa elegant, unachohitaji ni kujua namna ya kuufanya muonekano wako uonekane katika hali nzuri.

Mfano mzuri ni uchaguzi wa viatu hivyo kama ni mpenzi wa flats basi nunua ambazo zina rangi na design nzuri, huwezi kuvaa sandals ina midoll au rangi kali na vazi la maana na ukanonekana vyema lazima viatu vitashusha vazi hilo, sio kwasababu ni sandals bali ni design na uchaguzi wa rangi za viatu hivyo.

Leo tupo na mwanamitindo na fashionista Julitha Kabete ambae tumemuona mara nyingi akiwa amevalia flat sandals na kuonekana amependeza

kama unaenda sehemu za ufukweni au sehemu za ku-swim basi unaweza kuvaa piecez zako nzuri uka style vyema na ukavaa flats zako kama Julitha hapo chini

Kwa wale wa casual outings kwenda movies, running errands au shopping kwenye basi unaweza kuvaa suruali yako iwe jeans au material yoyote na ukamalizia muonekano wako na flats.

Kwa mitoko muhimu kiasi kama kwenda kula lunch, brunch, dinner za kawaida na marafiki unaweza kuvaa vazi lako linaloendana na sehemu unayoenda na ukamalizia muonekano na flats zako.

Well kikubwa kuhusu kuvaa flats ni kuhakikisha miguu yako misafi, umepaka mafuta vyema na kucha ziwe safi lakini pia hakikisha flats zako zinaendana na mavazi yako.

Related posts