Wengi tunamjua International Model, Flaviana Matata ni moja kati ya wanamitindo ambao wanafanya vizuri kutoka Tanzania. Flaviana amezaliwa na kukulia mkoani Shinyanga, lakini si Msukuma, Baba wa Flaviana ni myambo kutoka Karagwe that makes Flaviana myambo pia.
Amesoma Shinyanga Primary School, secondary amesomea Girls Mission Secondary School, hakuendelea form five na form six akaamua kwenda chuo ambapo alisomea electrical engineering, tunaweza kusema kama Flaviana asingekuwa model leo basi angejulikana kama fundi umeme, wakati amemaliza chuo na ku-graduatem Flaviana alishawishiwa kwenda kushiriki Miss Universe ambapo alienda na kushinda Miss Universe ya kwanza kufanyika hapa Nchini Tanzania mwaka 2007, baada ya kushinda Miss Universe matokeo yalitoka na alikuwa na option mbili ya kuendelea na shule au kuendelea na modelling ambapo yeye aliamua kufanya modeling kuwa career yake na kutokuendelea na shule.Mwaka huohuo 2007 Flaviana alienda kushiriki Miss Universe World ambapo aliingia katika 15 semifinalists lakini aliweza kuingia katika 6 bora kwenye evening gown competition.
Flaviana amelelewa na baba ambapo mama yake alifariki katika ajali ya Mv Bukoba mwaka 1996, tukirudi nyuma miaka hii ya 2000 wazazi na familia nyingi hazikuwa zinachukulia modelling kama kazi ya maana wengi walikuwa wanaona kama uhuni kwa yeye kuweza kuchagua modeling over kitu ambacho amesomea kilikuwa kitu cha uthubutu sana, na tunaona hapa kwamba alikuwa na passion na modelling na ndio maana akaamua kuacha pembeni electrical engineering na kuingia katika modelling career.
Wakati angeweza kuendelea na shule na kupata kazi yeye aliamua kukuza career yake ya modelling ambayo alikuwa na passion nayo, hatusemi wengine wa drop out schools kwa kuwa wana passion na kitu fulani ila tunasema kwamba unaweza kufanya kile unachokipenda kwa nguvu na kinaweza kuleta positive results, kuliko kupoteza muda kufanya kile ambacho huna mapenzi nacho moyoni, Flaviana anaweza kuku-inspire katika hili labda leo asingekuwa na Flaviana Matata Lavy Products ambayo hii ni kampuni yake ya rangi za kucha au kuwa na Flaviana Matata Foundation ambayo husaidia watoto yatima wakike katika elimu zao.
Lakini pia kupitia modelling Flaviana ameweza kushinda Tuzo mbalimbali ambapo labda angekuwa electrical engineering asingeweza kuzipata hzi tuzo
- 2011: Model of the Year, Arise Fashion Magazine Awards
- 2012: Outstanding Female Model Of The Year, Nigeria Next Super Model Awards.
- 2012: Face Of Africa, Africa Diaspora Awards
- 2013: Humanitarian Of The Year, Swahili Fashion Week Awards
- 2016: Arts And Culture (Lavy Products), Clouds Fm Malkia Wa Nguvu Awards.
Lakini si hivyo tu Flaviana ameweza kutembea katika runways za wabunifu wa kubwa Nje na Ndani Ya Nchi kama Mustafa Hassanali, Vivienne Westwood, Tory Burch, Suno, Macy and Louise Gray .Tommy Hilfiger, Jason Wu, Rachel Roy, Charlotte Ronson, Charlotte Ronson, Holly Fulton, Sally LaPointe, Alice Ritter, Todd Lynn among others and has featured in the Alexander McQueen film tribute.
Flaviana pia amekuwa featured katika magazeti makubwa ya fashion kama Marie Claire, French Revue De
Modes, Essence, Nylon magazine, Arise Magazine, FA Japan, the Hunger editorial, The Vision (magazine) – China, Grazia Italy and UK, Elle magazine, Schon magazine, she has also featured in the magazines Dazed & Confused, Glass Magazine, L’Officiel and i-D Magazine.Matata is currently signed by Wilhelmina Models.
Mwka 2013 she was listed by Forbes Africa as one of the top seven models to have recorded the highestincome in Africa, Wakati mwaka 2017 alikuwa mentioned na okay.com kama mmoja kati ya Top 100 Women in Africa.
Flaviana chose to building her own career over having a job. Be Inspired
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/flaviana-matata-is-a-true-definition-of-passion-is-the-difference-between-having-a-job-and-building-a-career/ […]