Tunapenda kuona watu maarufu wakiwa wamevalia kitu kiancho fanana, well no sio kwasababu ya kuwalinganisha ila ni kwa sababu ya kupata option nyingi za kuvaa hilo vazi lakini pia kujua nini kina trend, na kwa sasa hizi two pieces za flare skirt na off shoulder top zenye rangi mbalimbali zinaonenekana kutrend sana sio tu kwa Hamisa Mobetto na Julitha Kabete tumewaona fashionista’s mbalimbali wakivutiwa na two pieces hizi`

Tulimuona fashionista Julitha Kabete akiwa amevalia two pieces hizi zenye rangi ya blue, kijani na nyeupe kutoka kwa divaboutiqueonline.com, alimalizia muonekano wake na simple makeup huku akiwa ameachia nywele na flat sandals.

Hamisa Mobetto yeye alivaa two pieces hizi zikiwa zinarangi nyingi nyingi kama orange, blue na nyeupe na yeye amemalizia muonekano wake na simple makeup look, sandals huku akiwa ameachia nywele

Unaweza kupata two pieces hizi kwenye blog ya diva boutique lakini pia tumeziona kwenye collection za wabunifu wetu wa hapahapa Tanzania akiwepo Lucky Design

Na Bijoux Trend unaweza kutembelea page zao kujua zaidi

lakini pia tuambie umeona nani amependeza zaidi na haya mavazi kati ya Hamisa na Julitha?