Video director kutoka Tanzania anajaribu kutuambia tutegemee kumuona Jux mnyamwezi kila siku, kwa maana tumezoea kumuona Jux akipendeza kwahio tunaweza tusimuone Jux akiwa ameigiza kama choka mbaya kwenye video zake za muziki. Hanscana alipost video ya Jux iitwayo zaidi ambayo alifanya nae na according to Hanscana, Jux alitaka kubadilika kidogo katika video hii na kuigiza choka mbaya lakini yeye alishauri avae tu kinyamwezi
Ikabidi tupitie comments tuone wanazengo wanasemaje ambapo kuna huyu mmoja ambae aalivutia macho yetu kwa comment zake, akisema kwamba inabidi location na uimbaji wa mtu uzingatiwe, yaani Jux anaimba nyimbo classic location haiweze kuwa uswahilini huku Hanscana akisema kwamba location imebidi iwe uswazi kwa maana idea ya video ni kwamba Jux amefall in love na msichana wa uswahilini
Kwetu sisi tunadhani hakuna msanii ambae anaweza ku-maintain awe wa aina fulani video zake ziwe hivi, msanii anatakiwa kuwa dynamic awe anabadilika badilika kuendana na mazingira yanavyo muhitaji. Jux ilibidi avae uhusika alio utaka tumuone akiwa tofauti, tumesha muona akiwa anapendeza classic kwenye video zake zote, yeye mwenyewe kutaka kuuvaa uhusika wa uswazi lilikuwa wazo zuri sana na angetu-surprise sana, tungepata kuona upande wa pili wa Jux. Afromates Ninyi mnaonaje? Hanscana yupo sawa au hapa amepotea?
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/hanscana-anatuambia-tutegemee-kumuona-jux-mnyamwezi-kilasiku/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/hanscana-anatuambia-tutegemee-kumuona-jux-mnyamwezi-kilasiku/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/hanscana-anatuambia-tutegemee-kumuona-jux-mnyamwezi-kilasiku/ […]