SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Happiness Magese  Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish
Mitindo

Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish 

Kwa wanawake warefu huwa ni shida kidogo kupata nguo zinazo wafaa ambazo ni stylish na hii hutokana na kwamba brands nyingi za mavazi huwa zina consider kimo fulani cha binaadamu na kusahau wale wengine ambao wamejaaliwa urefu au mwili mkubwa. Hivi karibuni mwanamziki Megan Thee Stallion alitangaza kufanya collab na Fashionnova kwa ajili ya kutoa mavazi ya wanawake warefu maana wanapata tabu.

Anyways back to Happiness Magese ambae yeye alishawahi kutwaa Taji la Miss Tanzania 2001 Ni moja kati ya wadada warefu tuliojaaliwa nao Tanzania. Tofauti na wadada wengine Happiness pamoja na urefu wake lakini ni moja kati ya wadada wanaopendeza sana na mavazi yao na leo tumejaribu kuangalia Tips chache kutoka kwake ku-share na wengine ambao ni warefu na hawajui wafanyaje

  • Flare / Wide Leg / Straight Pants

Hizi ni nzuri kutokana na miguu mirefu ambayo watu warefu wanayo, ili kutokuichora na kuonekana mirefu mno ni vyema kutumia suruali ambazo chini ni pana kidogo hazikamati miguu.

  • Volume / Color & Print

Mwili wako una uwezo wa kuhimili hivi vitu vitatu, kwahio vaa hivi vitu kadri uwezavyo, vaa rangi ambazo ni bold, prints na unaweza ku-layer vile upendevyo lakini kuwa makini katika volume hapa usi-over accessories au kutumia fabric ambazo ni nene.

  • High Necklines

Hasa ikiwa wewe ni mwembamba, kuvaa mavazi ambayo shingo yake ni ndefu mfano: high-cut blouses, turtlenecks, na halter ni nzuri kwa sababu itasisitiza urefu wa shingo na kukupa muonekano mzuri

  • Break It Up

Unless unataka kuonyesha urefu wako unaweza kuvaa bila ku break-up look lakini kama ungependa kuonyesha utofauti katika mwili wako ni vyema uka-break up look yako, unaweza kuvaa belt au rangi tofauti juu na chini ili kupata proportion.

Well Afromates ni matumaini yetu tumeweza kukupa Tips chache za nini ufanye kama ni mrefu, tupe maoni yako hapo chini.

Related posts

3 Comments

  1. pop over to this site

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/happiness-magese-akionyesha-wanawake-warefu-namna-ya-kuwa-stylish/ […]

  2. old pillsbury cookie recipes,

    … [Trackback]

    […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/happiness-magese-akionyesha-wanawake-warefu-namna-ya-kuwa-stylish/ […]

  3. Booth fabrication company

    … [Trackback]

    […] There you can find 96054 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/happiness-magese-akionyesha-wanawake-warefu-namna-ya-kuwa-stylish/ […]

Comments are closed.