Mamia ya watu walikusanyika Chato mkoani Geita Tanzania, kumzika aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk John Pombe Magufuli. Ambapo kulikuwa na watu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali walioenda kumsindikiza katika safari yake hii ya mwisho.
Katika waombolezaji hawa kulikuwa na watu maarufu kama Diamond Platnumz, Lulu Diva, Rayvanny na wengine wengi, tupo hapa kuangalia je mionekano yao iliendana na sehemu waliyoenda?
- Stealing Attention
Tuanze na Diamond Platnumz ambae yeye alikuwa amevalia vazi la suit nyeusi na shirt nyeupe ndani, alikuwa msafi na presidential look. Tatizo letu na yeye au tuseme asilimia kubwa ya watu maarufu hawa ni over accessorizing, Diamond alikuwa na kofia, miwani, cane ( Fimbo), Bow tie ni kama alikuwa anaenda kwenye red carpet badala ya msibani tunadhani next time ajifunze kuhusu kuwa minimum na kuto steal the attention msibani pia Bow tie na red tie hazifai kuvalia masibani.
- Over Accessorizing
Lulu Diva ni msanii wa kike ambae nae alionekana kuhudhuria mazishi haya, yeye alimuwa kuwa classy akiwa amevalia gauni nyeusi pamoja na fascinator nyeusi tumependa muonekano wake lakini bado tunarudi kwenye accessory, tunadhani angevaa tu study earrings bila cheni ingekuwa bora zaidi. Ukiachana na hivi viwili alikuwa amevaa vyema kuendana na msiba.
Mwingine ambae tuliona alikuwa over accessorized ni Rayvanny, alikuwa amesukia yeboyebo na kuvalia babushka headscarf, Rayvanny anahitaji shule na tution kwaajili ya mavazi yake sio tu msibani bali katika maisha yake ya kawaida pia, tunadhani haikuwa inachukua nusu saa kufumua hizo yebo angewaomba Zuchu na Darleen wakamsaidia kufumua hii ingeepusha kuvaa hio Babushka msibani na ku-draw attention.
- Suit Attire Msibani
marioo, Chegge, Goodluck Gozbert As much as tungependa kuongelea kuto kuvaa suit au tuxedo msibani tunaweza kusema “msiba ulikuwa mkubwa wengi wetu tiliona suit ndio choice nzuri kutokana na hadhi ya msiba” wakati mwingine au msiba mwingine mkubwa kama huu ukitokea mnaweza kuvaa tu suruali ya kitambaa shirt ya dark color, dark solid neckties na moka zenu safi bado mkawa smart kwaajili ya msiba na kutokuchukua attention kubwa.
- Proper yet stylish
Tumewaona wasanii ambao walikuwa proper na mazishi, Gnako ambae alivaa full black japo tunatamani angemalizia kufunga vifungo kutokuacha kifua wazi,
Jux alivaa vyema bila ku-draw attention walakuwa too much pamoja na Cyrill Kamikaze tunadhani hawa ni mfano tosha endapo kutatokea msiba mwingine mkubwa tutajua nini cha kuvaa

Note: Lengo ni kujifunza namna ambavyo unaweza kuvaa mavazi yako vyema hasa katika misiba mikubwa ya ki-Taifa kama hii, Dunia inatuangalia inabidi tujue nini cha kuvaa ilikutokuenekana wa ajabu au kuongelewa vibaya.
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/how-celebrities-attended-the-late-hon-magufuli-funeral/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/how-celebrities-attended-the-late-hon-magufuli-funeral/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/how-celebrities-attended-the-late-hon-magufuli-funeral/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/how-celebrities-attended-the-late-hon-magufuli-funeral/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/how-celebrities-attended-the-late-hon-magufuli-funeral/ […]