SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

How To Elegantly Hold (Carry) A Clutch
Mitindo

How To Elegantly Hold (Carry) A Clutch 

Unamtoko wako wa kubeba clutch unayo nzuri umevaa mavazi yako vizuri umependeza hasa, lakini sasa unabeba ile clutch kama unabeba gunia au handbag ya kazini au ya kwendea clinic.

Clutch ni bags ndogo na usually ni classy bags maana ni za mitoko hasa ya usiku, dinner, red carpet, mitoko fulani huitaji vitu vingi.

Leo tunakuletea namna ambavyo unapaswa kubeba clutch yako,

Kwanza kabisa clutch ina bebwa mkono wa kushoto, ili kuupa nafasi mkono wa kulia kufanya vitu vingine kama kutoa salamu etc.

Kuna namna kadhaa za kubeba clutch

  • Ishikilie Kwa Mbele

Shikilia clutch mbele yako kwa mikono yote miwili na ncha za vidole zikielekeza chini. Hii ni njia ya kifahari ya kushikilia clutch hasa wakati umesimama.

  • Ishikilie Clutch Yako Kiganjani

Kama clutch yako ina mkono (handle), basi unaweza kuishikilia kiganjani, na hii ni namna rahisi unaweza kujiachia kutembea na kuonyesha vazi lako vyema

Ibebe Pembeni / Upande

weka tu kidole gumba nyuma ya mkoba wako na upumzishe vidole vyako vyote vinne upande wa mbele

Ishikililie Kwa Chini

Pitish kiganja cha mkono wako kwenye sehemu ya chini ya clutch na kufunika vidole vyako chini huku vidole vikiwa vinaangalia upande wa nyuma na kidole chako gumba kikiwa mbele.

Well tuambie ni namna gani huwa unabeba clutch yako?

Related posts