SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

How To Repeat Outfit Without Getting Noticed
Mitindo

How To Repeat Outfit Without Getting Noticed 

Inawezekana una mavazi machache au unayo mengi lakini unapenda kurudia mavazi yako, ikiwa Dunia inatupelekesha kuamini kwamba kurudia nguo ni jambo la ajabu tupo hapa kukwambia ni sawa kurudia nguo, Lakini je unazirudiaje ili watu wasijue kama umezirudia? Leo tunakuletea tips chache za nini ufanye kurudia vazi lako na usijulikane

Kuwa mbunifu na combination zako

Kama unavaa vazi moja kilasiku na viatu vilevile, mkufu uleule, handbag ileile ni rahisi kugundulika kwamba umerudia vazi lako, jaribu kubadilisha combination zako mara kwa mara. Mfano una floral shirt ina maua mekundu, kijani na nyeupe basi jua unaweza kuvalia suruali za rangi hizo na hio blouse usivae na rangi ya kijani kila mara, unaweza kuvaa nyeusi, unaweza kuvaa nyekundu au nyeupe na hapo utakuwa umeweza kurudia nguo yako bila ya watu ku-notice.

Badilisha Style Ya Nywele

Unaweza ukawa unajaaribu kila siku kumix your outfit na ukawa unaonekana unarudia nguo kila siku. sio mbaya kitu cha muhimu unachotakiwa kufanya ni kujitaidi kubadilisha muonekano wa nywele zako unaweza kucheza na nywele zako jinsi unavyotaka mara leo umebana, kesho umeachia itakusaidia uonekane mtu unayebadilika kila siku hata kama ukiwa unarudia nguo.

Jaribu Kuvaa Accessories

Hiki ni kitu cha muhimu sana kama mtu wa kurudia sana nguo basi jaribu kuongezea accessory kwa sababu zitawafanya watu wazingatie sana accessory zako na kutofocus na outfit. kitu cha muhimu ni kuadd accessory but keep jewely simple yani usiweke vitu vingi, add accessory ambazo zitakufanya uonekane smart unaweza ukaadd earing, bracelet, necklace.

Layering is everything

unaambiwa hivi layering is an art na kama unavyojua hakuna art ambayo haina faida. kitendo cha kuongezea shirt, scarf, sweater katika outfit yako itakufanya ubadilishe kabisa muonekano wako na kukufanya uwe perfect,kama unampongo wa kurudia outfit yako basi jitaidi sana kufanya layering.

Badilisha Handbags

jitaidi sana kubadilisha hangbag yako itakufanya usionekane unarudia outfit. ukiwa na mikoba mingi basi itakufanya uwe na choice nyingi kama unaweza basi jitadi sana kila ukichange handbag iwe inaendana na kitu kimoja kwenye outfit yako.

Badilisha Viatu

haijalishi umevaa same outfit mara ngapi lakini ukijitaidi kubadilisha kiatu chako katika hiyo outfits itakufanya uonekane mpya. kitendo cha kubadilisha kiatu kitakufanya ubadilishe muonekano wote na wataalamu wa mambo ya mitindo wanakuambia kila siku (the shoe closes your appearance) so jitaidi kubadilisha kiatu itakufanya uonekane tofauti kama ulikuwa unavalia mules unaweza ukachange ukaanza kuvaa na high heels au flats.

Know Your Audience

najua unaweza ukawa unapenda kurepeat outfit kwa sababu unaambiwaga unapendeza sana but cha muhimu ni kujua audience yako ni watu wa aina gani kama umevaa kwenye birthday party basi usivae tena kwa watu wa aina iyo jitaidi sana ukavae katika different place hii itakufanya usionekane unarudia nguo.

Note; ukiona unashinda kufanya hivyo vyote basi usisumbuke sana unaweza kuadd jacket na itakufanya usiwe noticed. kurudia nguo sio vibaya ila kushindwa kustyle outfit yako ndio kitu kibaya ni matumaini yetu umetuelewa na itakusaidia katika kubadilisha muonekano wako.

imeandikwa na @gotchathegreatest

Related posts