SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Husna Tandika & Kiara Sheba Ni Kweli Wabunifu Wanaigiana Kazi?
Mitindo

Husna Tandika & Kiara Sheba Ni Kweli Wabunifu Wanaigiana Kazi? 

Katika kutafuta jibu la malalamiko ya wengi kwamba wabunifu siku hizi wanaigiana kazi na kwamba kwa sasa wabunifu hakuna kuna ma fundi cherehani ili bidi tuhoji pande zote mbili kwa wadada na wakaka, tumesha ona majibu ya Martin Kadinda  na samuel zebedayo lakini je wadada wao wana maoni gani na hawa ni Kiara Sheba Na Husna Tandika na maoni yao kuhusu swala hilo

Afroswagga: Dada Husna wewe una liongeleaje hili swala la wa Tanzania kusema ” Tanzania hamna wabunifu bali kuna mafundi cherehani”

Husna TandikaKuhusu fundi Cherehani ilo sijaelewa kwanini wanasema hivyo, maana nnavyojua wabunifu wengi hawajuagi kushona. Rather wako karibu na mafundi but sio washonaji

Afroswagga: Vipi Kuhusu kuigana kazi?
Husna Tandika: Ni kweli wengi wanaigizana sana kazi, na mara nyingi sana inatokea kutokana na wateja wengi  wanapenda kuvaa nguo ambayo imevaliwa na star. Then kila mtu atataka that look.
I once mvisha jokate, nilipata wateja wengi mno ambao walitaka kuvaa kama nguo yake… Baadhi yao without even knowing was my design
Pia unakuta wateja wengi wanakuja kwa mbunifu wakiwa na picha zao. As in “nataka unishonee kama lulu, au nataka unishonee kama Wema / Mobetto nk”
So ni mawili either ufanye anachotaka mteja au umpe ushauri na ubuni wewe kitu kingine au similar but unaweka kitu cha kufanya brand yako ijulikane
But just kumalizia ni kwamba mbunifu anafanya more than one job kuliko kukaa na kubuni nguo. Yeye ni marketing, hr,  mshauri, accountant etc. Reason why wengi wanakosa ile creative mode.

Lakini pia tulifanya mahojiano na mbunifu Kiara Sheba na yeye alikuwa na haya ya kusema

Kiara Sheba: Wabunifu wapo.Kinachofanya watu waseme kua hamna wabunifu ni mafundi cherehani kujiita wabunifu bila kuzingatia vigezo vya ubunifu. Kibongobongo pia ubunifu unachukuliwa poa, inaonekana ni fani ambayo mtu yeyote anaweza fanya.Lakini kiukweli ubunifu ni fani ya kuumiza kichwa sana ili kupata mawazo mapya na mitindo mipya.


Kuhusu kuigana kazi..Kiukweli kuna ukweli uliopo kwenye hilo. Ukizingatia fundi cherehani wengi wanajiita wabunifu. Na kwa kuwa hawana ubunifu kunakua na copy paste nyingi. Hii inarahisishwa na utandawazi, kila kitu kipo mitandaoni kwahio kudesa ni rahisi mno. Lakini pia kuna kitu wenye ubunifu kinaitwa misimu. Misimu inakua na rangi na mitindo inayofanana, kwa mfano sahivi mitindo ya miaka ya 80 iko kwenye fashion kwahio unakuta wabunifu wanabuni nguo wakiwa na hilo kichwani.
Kwahio sa zingine sio kuigana ni kufuata trends

Related posts

6 Comments

 1. Extra resources

  … [Trackback]

  […] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/husna-tandika-kiara-sheba-ni-kweli-wabunifu-wanaigiana-kazi/ […]

 2. why not check here

  … [Trackback]

  […] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/husna-tandika-kiara-sheba-ni-kweli-wabunifu-wanaigiana-kazi/ […]

 3. Ventilare

  … [Trackback]

  […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/husna-tandika-kiara-sheba-ni-kweli-wabunifu-wanaigiana-kazi/ […]

 4. Where in Oregon can I get magic mushrooms?

  … [Trackback]

  […] Here you will find 52430 more Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/husna-tandika-kiara-sheba-ni-kweli-wabunifu-wanaigiana-kazi/ […]

 5. 웹툰 사이트

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/husna-tandika-kiara-sheba-ni-kweli-wabunifu-wanaigiana-kazi/ […]

 6. pgslot

  … [Trackback]

  […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/husna-tandika-kiara-sheba-ni-kweli-wabunifu-wanaigiana-kazi/ […]

Leave a Reply