SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ifahamu Lady Dior Bag Aliyozawadiwa Vanessa  Mdee Na Mumewe Rotimi
Mitindo

Ifahamu Lady Dior Bag Aliyozawadiwa Vanessa Mdee Na Mumewe Rotimi 

Kwenye kurasa zake za Instagram yake Vanessa alipost short video clip ambayo inamuonyesha mumewe Rotimi akimkabidhi zawadi ambayo aliifungua ndani na kalikuwa ka handbag kadogo tu keusi ka Dior, lakini exciment ya Vanessa ilikuwa kubwa sana wengi itakuwa tumejiuliza kwanini?

Handbag hii ilibuniwa mwaka 1994 na mbunifu Gianfranco Ferre ambe alikuwa inspired na Napoleon III chairs ambazo zilitumika katika show ya kwanza ya kampuni hio mwaka 1947. Handbag hii mwanzano ilikuwa inaitwa Chouchou ambapo ni neno la French linalo maanisha favorite.

Mwaka 1995 Bernadette Chirac alimzawadia handbag hii Princess Diana ambae aliipenda na akataka atengenezewe hii handbag kwa rangi nyingine tofauti tofauti, na alionekana kuiibeba hii handbag mara kwa mara ikiwepo mwaka 1996 katika red carpet za Met Gala na hapo ndipo jina la Lady Dior lilipopatikana.

handbag hii imekuwa ikitengenezwa kwa kubadilishwa material na rangi mara kwa mara na ni moja kati ya Iconic handbag kutoka katika kampuni hii ya Dior, kwa sasa inauzwa Eur 4,800 sawa na tsh 12,383,522.40 wakati pre owned zinaanzia kuuzwa usd 3,459 sawa na Tsh 8,128,653.46 za ki-Tanzania.

Related posts