Kumekua na malalamiko mengi katika sekta ya mitindo, wana mitindo na wabunifu wengi walio pita na waliopo wana lalamika kwamba Sekta hii haipewi support si sawa na sekta nyingine kama muziki na filamu. Ni kweli imekua hivyo kwa miaka mingi sasa ni kutokana na tabia mbaya za wachache zina wagharimu wengine, watu wengi wanaona sekta ya mitindo ni uhuni na kwa sasa ime zidi kutokana na watu wake kuto jiheshimu tumeona wana mitindo mbali mbali wakiwekwa kwenye magazeti kwa kashfa mbalimbali mbaya, na wengi hufanya hivi kupata kiki (kama ambavyo wenyewe husema) wana taka kupata jina na kutambulika mjini kwa sababu tu ukiwa na jina ndio watu wengi wata kupa kazi ufanye, hawezi kupewa kazi fulani mtu asiye na kiki kwa makampuni hudhani mtu mwenye kiki kwa wakati huo ata waletea wateja kuliko yule ambae hana kiki. Kiupande mmoja ni kweli na upande mwingine wana kosea, Vipi wana kosea? tunawaona watu kama Flaviana Matata, Hapiness Magesse, Miriam Odemba au Herieth Paul kwa hapa kwetu Tanzania wanajulikana lakini si sana ila huko nje wana fanya kazi nzuri sana makampuni wange fikiria pia ukimtumia Happy au Miriam hutopata tu wateja kutoka Tanzania Bali pia Nje ya Tanzania.
Turudi kwenye kushirikiana ni kweli sekta hii haipewi support labda na makampuni, magazeti na hata serikali lakini Je? wao waliopo tayari katika dira ya mitindo au wamesha julikana wana wasaidia vipi wengine wanao jaribu kuingia katika ulimwengu huo? au hata wao wenyewe kwa wenyewe wana saidia vipi katika miradi yao? mtu kama Hapiness ana mradi wake kwa sasa lakini ni wana mitindo na wabunifu wachache sana wanao msupport, huwezi kulalamika hupati support kama nyinyi wenyewe kwa wenyewe humpeani hio support, kama mngekuwa mna shikana katika mambo mbali mbali wengi wange ona na wange wapa support kilio cha mtu mmoja si sawa na kilio cha wengi, kilio cha mtu mmoja ni sauti lakini kilio cha wengi ni ujumbe ambao utasambaa kwa kasi mno.
Mpo wengi sana kwa sasa ambao mna miradi yenu mnge anzisha hata chama na kuanza kufanya miradi kwa pamoja hii tu haito saidia ninyi kusikika bali pia kusaidia wale wanao chipukia kujitambua kwamba bila hata ya mie kukaa utupu au kutafuta kiki kwa njia mbaya ninaweza kufikia malengo kama ambao walio tangulia kwa kujiunga nao na kufanya nao kazi.
Related posts
7 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you will find 88494 additional Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/inawezekana-kama-tu-mtashirikiana/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/inawezekana-kama-tu-mtashirikiana/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 14178 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/inawezekana-kama-tu-mtashirikiana/ […]
… [Trackback]
[…] Find More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/inawezekana-kama-tu-mtashirikiana/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/inawezekana-kama-tu-mtashirikiana/ […]
… [Trackback]
[…] Here you will find 93597 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/inawezekana-kama-tu-mtashirikiana/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/inawezekana-kama-tu-mtashirikiana/ […]