SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Its African Designers Time, From Beyonce, Janet Jackson, Tyra Bank And Many More
Mitindo

Its African Designers Time, From Beyonce, Janet Jackson, Tyra Bank And Many More 

Tuko hapa tukiangalia namna ambavyo wabunifu kutoka Nchi za Africa yaani majirani zetu wakiwavalisha watu maarufu wakubwa wenye influence kubwa Duniani, wakati sisi tukiendelea kuwa ndugu watizamaji. Kama ulikuwa hujui basi ngoja tukujuze, mwaka huu umekuwa na revolution kubwa kwa watu maarufu kutoa support kwa wabunifu wadogo na wakubwa kutoka Africa, kuna movement ambazo zipo kama #wearafricadesigns au #buyblackowned na hii ni kutokana kuonekana wa-Africa kuto kutoa support kwa wa-Africa wenzao na kupelekea kutajirisha wengine huku wakiwaacha ndugu zao wakiendelea kusota na kunyanyika.

Hii imeonekana sio tu katika vyakula na mambo mengine lakini hata katika fashion pia, seems like everybody is woke na kila mtu anataka mwingine nae anyanyuke, Nchi nyingi zimefanikiwa na movement hii, from Nigeria,Senegal,  Cameroon, South Africa na kwingineko ,

Katika event kubwa ya global citizen festival katika mavazi yake mwanamziki Beyonce katika mionekano yake alichagua kuvalishwa na wabunifu wadogo kutoka Africa ambapo usiku ule akiwa ana perform alivaa green outfit kutoka kwa South Africa Fashion brandEnhle Mbali Maphumulo and Quiteria & George collaboration, Kama tungekuta hii design kwenye duka definitely  tunge shout a Beyonce look, that embellished body suit, and extra designed cover up was a statement of the outfit.

Hivi karibuni tumemuona mwanamuziki na muigizaji Kelly Rowland ambae alikuwa kundi moja na Beyonce “Destiny’s Child” akiwa amepost picha katika instagram yake akiwa amevalia yellow & blue two pieces za kitenge kutoka kwa mbunifu Tehilah Abakasanga  kutoka brand iitwayo ÖFUURË inayotoka Nchini Nigeria, she paired her look with statement earrings & box braids, like a true African woman

Mwanamitindo Tyra Banks na yeye tumemuona akiwa amepost hii picha katika Instagram yake akiwa amevalia kitenge top kutoka kwa brand ya UberStyle Woman kutoka Nigeria,

Lakini pia katikati ya mwaka huu tulimuona mbunifu Claude Lavie Kameni Kutoka Cameroon Alivyoweza Kumvalisha Janet Jackson Na Tracee Ellis Ross, Wakati Janet alimvalisha katika video ya wimbo wake mpya wa  Made For Now ambapo wimbo huu ulikuwa kama kurudi kwake katika game baada ya kuolewa, na kujifungua, ilikuwa ni big deal sio tu kumvalisha Janet bali kumvalisha kwa kipindi muhimu kama icho na to think that video itaendelea kuishi milele

Lakini pia aliweza kumvalisha mchekeshaji na muigizaji Tracee Ellis Ross katika American Music Awards na Tracee alikuwa host wa siku hio, ambapo aliamua kuvaa design za wabunifu weusi na Lavie alikuwa mmoja wao

Ni matumaini yetu tutamuona msanii mkubwa akiwa amevalia product kutoka kwa wabunifu kutoka Tanzania

 

Related posts

1 Comment

  1. Buy DMT online Melbourne

    … [Trackback]

    […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/its-african-designers-time-from-beyonce-janet-jackson-tyra-bank-and-many-more/ […]

Comments are closed.