Kwa miaka mingi wabunifu kutoka Tanzania wamekuwa wakilalamikiwa kutokuwa creative, wengi wame stuck na mitindo ile ile ya siku zote, ukiangalia collection zao nyingi zinafanana kasoro rangi na vitambaa, wengi hawapo tayari kuwa na ujaribu na mwishoe wana end up kuwa kwenye comfort zone yao, hii inatupelekea katika sekta ya ubunifu tupitwe kila siku na Nchi nyingine.
Well Muigizaji na sasa mbunifu Jacqueline Wolper anaweza kuwa mbunifu ambae Tanzania inamuhitaji endapo tu atakuwa tayari kujifunza zaidi, kwanini tunasema hivi? Jacqueline wakati bado hajajiingiza kuwa mbunifu alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao wanavaa wanapendeza, anajua kujipangilia na hii ni mpaka sasa, style za Jacqueline si hizi ambazo tumezizoea kutoka kwa wasanii wengine yaani kuvaa manguza au trending pieces hapana, yeye ana style kitu cha kawaida na kukipa muonekano mwingine kabisa extra.
Well tulipenda awe stylist lakini mwenyewe amechagua ubunifu which we can’t complain ana fanya kazi nzuri, ana beautiful & unique pieces, japo kuna wakati ana kosea which we all do as she is a human too. Sisi tungependa Jacqueline ajifunze kuhusu body types hapa panampiga chenga sana, mara nyingi ana buni mavazi kwa watu wenye body types mbali mbali vibaya as tumeona hii ikitoke kwa Aunty Ezekiel na Nandy, Nandy alimvalisha gauni ambayo alipaswa kuvaa Aunty na Aunty anamvalisha gauni za Nandy.
Lakini pia tungependa ajifunze kubunia wengine, Jacqueline ana jibunia mavazi ambayo yeye akivaa anapendeza lakini kumbe kuna tofauti ya mwili wake, rangi na jinsi ambavyo wengine wapo, kuna pieces kutoka kwake ambazo akivaa mwenyewe una sema Yes this piece is very beautiful lakini akija kuvaa mwingine ni tofauti kabisa, tungependa kuona ana umiza kichwa kufikiria na wengine pia sio kila kinacho mpendeza yeye na wengine kitawapendeza.
Anahitaji stylist Wolper ana weza kujistyle mwenyewe ilo halipingiki lakini ku-style wengine kwake ni ngumu ndio maana mara nyingi akimvalisha mtu mwingine anakuwa ana kosea kwa sababu tu hajui amvalishe kipi na kipi, anahitaji kufanya kazi na stylist na tunadhani akifanya hivyo pieces zake zitaonekana bora na vizuri zaidi kuliko sasa.
Ajifunze kujaribu vitu vingine Jacqueline aking’ang’ania kitu ame ng’ang’ania mwaka jana ilikuwa lace na black satin tumeiona the whole year na mwaka huu tunahisi hizi ruffle’s tutaziona mwaka mzima, tungependa kuona ana jitaidi kutafuta fabrics nyingine hasa pale anapo mvalisha mtu maarufu, tumechoka kuona same thing kwa kila msanii update you’re self.
As a designer tunadhani ana fanya kazi nzuri tunacho kipenda the most ni yeye kuwa tofauti na kuangalia wenzetu wana fanya nini, lakini pia tungependa kuona kama amependa design fulani na kuifanya basi abadilishe mtindo kidogo maana tuliona design zake zikigongana na design za wabunifu wengine na ina fanya watu waseme kwamba ana copy na ku-paste.
Hizi ni some of her beautiful design’s na unique tulizo zipenda akiwa amezivaa mwenyewe
The high slit cold shoulder kitenge dress
two pieces number
gold dress with balloon hands
Ruffles Ruffles
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Here you will find 45016 more Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/jacqueline-wolper-ni-mbunifu-tunaye-mtaka-endapo-tu-ataamua-kujifunza-zaidi/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/jacqueline-wolper-ni-mbunifu-tunaye-mtaka-endapo-tu-ataamua-kujifunza-zaidi/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/jacqueline-wolper-ni-mbunifu-tunaye-mtaka-endapo-tu-ataamua-kujifunza-zaidi/ […]
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/jacqueline-wolper-ni-mbunifu-tunaye-mtaka-endapo-tu-ataamua-kujifunza-zaidi/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/jacqueline-wolper-ni-mbunifu-tunaye-mtaka-endapo-tu-ataamua-kujifunza-zaidi/ […]