SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Hili Ni Jibu La Zuchu Kwa Miss Tanzania Organization?
Mitindo

Je Hili Ni Jibu La Zuchu Kwa Miss Tanzania Organization? 

Week chache zilizopita mwanamuziki Zuchu alipewa onyo na kampuni ya The Look ambayo inasimamia mashindano ya Miss Tanzania, Onyo hili lilitokana na mwanamuziki huyu kutumia Sash yenye maandishi ya Miss Tanzania, ambapo kampuni hio ilisema kuvaa Sash yenye maandishi hayo ni “kuiba na kupotosha utambulisho wa mrembo wa Taifa mwenye taji hili” na wakiendelea kusema kuwa ni ” kosa la kisheria kwa mtu yoyote kutumia jina hilo pasipo kutambulika na kampuni ya the look”.

Baada ya onyo hilo Zuchu ameonekana ku-post tena akiwa amevalia Sash hio huku akisema kuwa ni “Ndoto Ya Kila Mwanadada kwenye fani ya Urembo .Naamini kila Mrembo hutamani Siku Moja Kuja Kuwa Mrembo Wa Taifa (Miss Tanzania)

Ukiamini Katika Ndoto Zako Na Ukazipambania …Kamwe Hautoweza Kufeli Kila Jambo Linawezekana Kwa Kupambana Na Kumuomba Mungu 🙏🙏🙏”

Unaweza kujiuliza kwanini tumesema hili ni jibu kwao? well tulipost hili swala na kulikuwa na mawazo mbalimbali ambapo wengine walikubaliana na Miss Tanzania Organization huku wengine wakisema ni haki ya kila mtu kutumia sash hio kama ni m-Tanzania.

Unaweza kusoma maoni mengi kwenye post hapo chini kisha tuambie maoni yako kuhusu hili swala

Soma maoni zaidi hapa

Related posts