Tumekuwa tukisikia story za binti cinderella alivyo pendwa na mtoto wa mfalme, namna ambavyo Cinderella alikuwa ana teswa na masikini lakini akabahatika kupendwa na mfalme huyo, well wengi huwa tunachukulia hizi hadithi na kuzileta kwenye reality lakini tunasahau kuwa hata Cinderella alibadilisha muonekano wake siku hii.
Kiukweli namna unavyojiweka na ndivyo watu wakavyo vutiwa wewe, wanasema kila ndege utua katika mti wake, unavyoonekana ndivyo utakavyo wavutia wanao onekana kama wewe. Kama unaonekana affordable basi wenye value wako watakufuata na kama unaonekana valued ndivyo hivyo wanaoonekana namna yako watakufuata.

Kwenye story zetu Instagram mara nyingi huwa tunapata maswali kama Afro mimi sipati wanaume wa maana au kuna wale wengine wanaosema mimi wanaume hawanifuati kwasababu ni najipenda sana nahisi nawatisha.
Majibu yote haya mawili yapo kwenye muonekano wako, kuna wale ambao tunajiweka tu kawaida japo tunapenda kufuatwa na watu wa maana lakini hawatufuati kwasababu tu hawaoni kama ni level yao, na tunafuatwa na wale ambao wanaona ni level zao kwasababu tunaonekana wanaweza kutu-afford
Kuna wale ambao tunajiweka vizuri zaidi na wale ambao wanaona tuko high maintanance wanaogopa kutufuata, kama unaonekana ni high maintanance ni ngumu zaidi kufuatwa sababu wengi wanaona hawezi kuku-afford so until umpate yule ambae anaona anaweza kukujali kwa level yako akatokea ndio utapata umtakae.

Ni namna gani muonekano wako unaingia katika dating
- Your look affects first impressions and attraction
- Muonekano wako unaweza kuvutia aina fulani ya watu
- Muonekano waku unakupa confidence
Ni namna gani unaweza kutumia muonekano wako kupata watu uwatakao
Kuna hizo namna mbili hapo unaweza kuchagua ni yupi unataka kuwa, hapa tulikuwa tunaonyesha ni namna gani mavazi na muonekano yanaweza ku-athiri mahusiano yako inawezekana kuna watu wa namna fulani wanakufuata hujui kwanini, basi jua muonekano una play part kubwa sana kwenye dating cycle yako. Hakikisha una balance mavazi yako kupata watu uwatakao huwezi kuwa unataka wavaa suit wewe ukawa unavaa vijora ( sisemi haiwezekani lakini ni asilimia kumi kwa mia) wazungu husema look the party
Well tuambie je muonekano wako umeshawahi kuathiri mahusiano yako?
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…