SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Ni Mara Ngapi Unatakiwa Kununua Bra Kwa Mwaka?
Mitindo

Je Ni Mara Ngapi Unatakiwa Kununua Bra Kwa Mwaka? 

Kubadilisha sidiria yako mara kwa mara ni njia mojawapo ya kuepuka hatari za kuvaa sidiria isiyofaa/kukutosha, ambayo inaweza kukuletea athari za maumivu ya kichwa na maumivu ya mgongo kutokana na poor posture ya sidiria hio.

Kutokana na uchunguzi wa Harper Wilde, 70% ya wanawake walisema sidiria hukaa au kuvaa sidiria kati ya miaka miwili hadi mitano. Makala hii inaelezea kwa nini, jinsi gani, na wakati wa kubadilisha sidiria yako uipendayo na kununua nyingine.

  • Kwa nini huwezi kuvaa Sidiria moja milele?

Sidiria hutengenezwa kwa material ya kuvutika ambayo husaidia kutoa support kwa namna moja au nyingine, Sidiria lazima iweze kusogea na kujikunja kutokana na mwili unavyopelekwa, pamoja na kuyaweka matiti katika hali nzuri. Elastic inayowekwa kwenye sidiria inaruhusu hii kutokea, lakini sidiria inapoteza ufanisi na muonekano wake mara baada ya matumizi mengi, kama kufuliwa au kuvaliwa mara kwa mara, huchoka na hivyo hulegea na kupoteza ufanisi, pia kupungua au kuongezeka mwili kuna weza kusababisha upaswe kununua sidiria nyingine.

  • Ni mara ngapi unapaswa kubadilisha sidiria yako?

Hili ni swali rahisi, lakini jibu linaweza kuwa gumu kulingana na mara ngapi unatumia na kuosha/kufua sidiria yako, pamoja na ni kiasi mwili wako unabadilika. Hata kwa matumizi ya uchache na uangalifu, sidiria zote zitapoteza umbo lake baada ya muda kadiri nyuzi za elastic kwenye bendi na kamba zinavyoharibika.

Utafiti unapendekeza ubadilishe / kununua sidiria kila baada miezi 6-9, lakini inaaminika kuwa ikitumika kwa uangalifu sahihi, sidiria yako inapaswa kudumu muda mrefu zaidi.

Related posts