Imezoeleka ni wanamama ndio hupaswa kubeba mikoba, hasa kutokana na wao kuhitaji vitu vingi wakiwa katika mitoko yao, ukimuona mwanaume amebeba mkoba basi amemsaidia mwanamke kutokana na sababu mbalimbali. Lakini hivi karibuni katika collection za wabunifu mbalimbali ndani na nje ya nchi wameonekana ku-include handbags za wanaume. Well mikoba hii ipo toka zamani lakini kwa sasa imeonekana kurudi kwa kasi kutokana na kwamba watu maarufu wengi wa kiume wameonekana kubeba lakini pia kama ambavyo tumesema imeonekana katika collection za wabunifu mbalimbali.
Hivi juzi tulimuoana mcheza kikapu Le Bron James akiwa amebeba mkoba kutoka kwa mbunifu “Mr. Thom” ambao unaitwa “Mr. Thom Alligator Bag” amabpo ali-style bag hii na short – pant gray suit akiwa amevalia na viatu vyeusi na socks ndefu, alipendeza sana na kuonekana unique kama ambavyo tunajua sio wanaume wengi wanaweza ku – dare kuvaa suit ya kaptula, he made a statement kwa kubeba mkoba huo ambapo wengi walionekana kuuongelea kwamba kwanini amebeba mkoba?
Lakini pia most stylish Rapper Asap Rocky yeye alionekana akiwa amebeba tote bag kutoka kwa Gucci, Asap yeye alikuwa more casual kwa ku-style bay yake hii na Gucci Cardigan, t-shirt nyeupe, blue jeans na ndula na socks nyeupe. Hii picha ilipostiwa katika page ya Gucci na mwanamziki French Montana alienda ku-comment ” Not with the bag vibe but everything else is fire”
Lakini pia tuliona mbunifu Ally Rehmtullah akiwa anabeba bags alizo zibuni mwenyewe kwa kutumia vitenge mara kwa mara,
Kwetu sisi kama afroswagga hatuna tatizo na mwanaume kubeba mkoba as long as umebuniwa kubebwa na mwanaume, tukimaanisha wanaume mikoba yao ona design ambazo tofauti zina less color na urembo na somehow unaweza kuiona kabisa imekaa kiume, lakini pia kuna fashion ya unisex katika karne hii wabunifu wamekuwa wakibuni vitu ambavyo vinaweza kuvaliwa na wanawake na wanaume. Mwisho wa siku its all about fashion, uelewa na kufanya kile ukipendacho
But let us know your views je ni sawa au lah?
Related posts
2 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/je-ni-sawa-mwanaume-kubeba-mkoba/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/je-ni-sawa-mwanaume-kubeba-mkoba/ […]