SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Stylist’s Kutoka Tanzania Wanafanya Kile Wanachokihubiria?
Mitindo

Je Stylist’s Kutoka Tanzania Wanafanya Kile Wanachokihubiria? 

Katika sanaa ambayo husahaulika Nchini Tanzania ni stylist, Stylist wapo wachache mno na hata waliopo pia na wao hawatupi zile ladha ambazo sisi tungependa kuziona, wengi wanaiga styles kutoka kwa ma stylist wengine lakini pia wanafanya kazi moja mbili wakipata jina wanapotea this makes us wonder je tasnia hii ina nini? kwanini ambao wana survive ni wachache na wale wale ambao tunawajua toka tangu tangu?

Its no lie kwamba sasa hivi tasnia ya mitindo inakua, kuanzia movies, waimbaji na  watu maarufu mbalimbali wanajitahidi sana kufanya kazi na stylist’s na tunaona ambavyo mionekano yao inabadilika wengine wakifanya vizuri na wengine bado 50/50 well ili mradi wanalisongesha gurudumu la mitindo lakini leo we have a question kwa hawa ma-stylist wetu “Do they practice what they preach”?

 

Kwetu tunadhani wengi hawafanyi hivyo, most of them hawa practice kile ambacho wanasema, kwetu ukiongelea a stylist tunategemea muonekano mzuri uanzie kwake, kwenye feed yake katika mitandao ya kijamii mpaka katika kazi yake lakini kwao ni tofauti kabisa, Unaweza kukutana na stylist ukajiuliza mimi nivalishwe na huyu? si bora niji-style mwenyewe, mionekano yao ya hovyo mpaka inakatisha tamaa ,okay kuna msemo wa fuata maneno yangu na usifuate matendo lakini sometimes practical is better ESPECIAL kwetu sisi wa-Tanzania ambao bado tuponyuma kwenye swala zima la mavazi

Tukija kwenye mitandao ya kijamii unakuta stylist page yake iko so dry kama jangwa la sahara, hapost kazi zake wala kujipost mwenyewe like dude we need to know unafanya nini na kama upo hai, utasikia whatsapp me or dm me bila kuona kazi yako why should i bother? give me something ili nije huko dm na kwingine na hata wakipost their pictures are Astaghafillurah, mbaya hata ku-invest kwenye wapiga picha pia inashindikana? shout out to Macrida Joseph & Joujou Nyaki kwenye hili wanajitahidi sana.

Lakini pia as a stylist tunatakiwa kujifunza kwako tupe hata vi tips vya hapa na pale, mteja sio aje tu umpendezeshe siku moja lakini hata akiondoka kwako basi awe anajua namna ya kujivalisha, stylist wetu wanachojua ni kupost fulani kavalishwa na fulani hakuna kutupa tips za nini wala nini we need to learn from you, hata kama kuna ambae hana uwezo wa kuja kufanya kazi na wewe basi atleast apate viwili vitatu kutoka kwako, educate us on styling lakini wa kwetu ni wamelala hadi kuwaamsha tunaona tutalala sie.

 

Related posts

3 Comments

  1. roof skylight

    … [Trackback]

    […] There you will find 34355 additional Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/je-stylists-kutoka-tanzania-wanafanya-kile-wanachokihubiria/ […]

  2. try here

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/je-stylists-kutoka-tanzania-wanafanya-kile-wanachokihubiria/ […]

  3. 카드단말기

    … [Trackback]

    […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/je-stylists-kutoka-tanzania-wanafanya-kile-wanachokihubiria/ […]

Comments are closed.