SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Unatakiwa Kutokujijali Baada Ya Kuolewa?
Mitindo

Je Unatakiwa Kutokujijali Baada Ya Kuolewa? 

Leo kwenye pitapita zetu huko mitandaoni tukakutana na hii video ya mwanadada kutoka Nigeria ambae anasema amekutana na mchepuko wa mume wake na aka-realize tatizo ni yeye.

Ukiendelea kusikiliza hii video anasema kwamba huyo mchepuko ni fine girl, anavyovaa, nywele zake na anavyojijali wakati yeye ana nywele zake za minyoosho toka January.

Well tulivyoona hii video ikatufanya tuwaze je ni sawa kujiachia kutokujijali sababu tu umeshaolewa yaani siku ya mwisho mwanaume kakuona umependeza ni siku yenu ya harusi baada ya hapo wewe na vijora vijora na wewe, na je ni sawa mwanaume kuto nje na kucheat kisa tu mwanamke wake kaacha kujijali? Kwanini asimwambie ajijali?

well tunadhani hiki kitu kinaenda both ways, kwa mwanamke na mwanaume pia

Inatakiwa tujue kwamba kuolewa hakubadilishi kitu ni kwamba umetoka kuwa single na sasa umeolewa, huitaji kubadilisha dressing code wala kuacha kujipenda, dressing up sio kwaajili ya mtu bali pia ni kwaajili yetu, kama zamani ulikuwa unajipenda ukamvutia mwanaume akuoe kwanini sasa hivi unajitupa? kwamba ulikuwa unavaa kuvutia mume na umeshampata inatosha?

Hata kama ni mke au mama unahitaji kuonekana vyema kwaajili yako mwenyewe, mume wako na watoto, chukua muda wako kusuka, kutengeneza kucha, dress up hata kama huendi mahali, nguo zako za kushindia ziwe safi.

As kwa mwanaume tunadhani alikuwa na uwezo wa kumwambia mkewe kabadilika na anaanza kupoteza mvuto kwake pretty sure mke angejitahidi kurekebisha tatizo lake.

Well let us know unafikiriaje kuhusu ili swala?

Related posts