SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Je Wabunifu Wetu Wanauwezo Wa Kuacha Legacy Katika Tasnia Ya Mitindo?
June 1961: Audrey Hepburn (1929 - 1993) stops for lunch on Fifth Avenue in New York during location filming for 'Breakfast At Tiffany's', directed by Blake Edwards in which she stars as Holly Golightly. (Photo by Keystone Features/Getty Images)
Mitindo

Je Wabunifu Wetu Wanauwezo Wa Kuacha Legacy Katika Tasnia Ya Mitindo? 

Wakati tukiendelea kufikiri kwa nini Tanzania haina hafla za mitindo za kila msimu, likatujia wazo la kwamba Je wabunifu wetu wanaweza kuacha Legacy katika Tasnia hii endapo wataamua kustaafu kufanya kazi hii? Kuna wabunifu wengi huko Nchi za wenzetu ambao wamestaafu kazi ya ubunifu lakini bado wanakumbukwa kwa kazi zao, bado kazi zao zinaishi, na kuna wengine ambao vitu vyao walivyo buni kabla ya kustaafu vinauzwa ghali sana kutokana na tu na ukubwa wa legacy yake. Je wakistaafu hawa wa kwetu hapa Tanzania kuna ambae atawakumbuka na kuendelea kununua mavazi yao?

Tunaweza kusema wabunifu wetu hawajafika huko bado kwa maana kufika huko kwenye kuacha legacy kunahitaji uwe creative na kazi yako, kazi yako isishuke thamani bali iwe inaendelea kupanda siku mpaka siku kitu ambacho sisi hatuna. Collection inakaa kwa mwaka mmoja au miaka kadhaa halafu inasahaulika hii ni kutokana na kwamba jicho letu limekaa sana katika trends na kuigana kuliko kufanya kazi ambayo inaishi.

Kazi yako inapokuwa sawa na ya mwengine tayari umeishusha thamani ile ya kwako na ya mwenzio kwa sababu tu inaonekana kitu kimoja ina ruhusiwa kuvutiwa na design ya mtu lakini don’t make it obvious kama umeiga na pia kama umeiga jaribu kuifanya iwe better version kuliko ya uliemuiga.

Lakini pia kuna kitu kinaitwa vitambaa ( kwa wenzetu huwa wanatafuta unique vitambaa or even create them themselves) kwetu wabunifu wanaenda kushop fabrics zao kariakoo kila mtu anaposhop. Kwanini nije kununua nguo kwako kama nina weza kukipata kitambaa kama chako na nikaenda kwa fundi juma kushona mshono kama wako? Hapo ndipo unapokuta collection ya mbunifu haikai zaidi ya miezi miwili imesha tapakaa mjini na kupoteza ladha. Ndio maana leo hii ukiona Fendi unajua hii Fendi, Ukiona  Balmain, Vercase wote wanajulikana kutokana na vitambaa vyao wana Signature Fabric ambayo ina watambulisha. Na ndio maana ikiwa fake inajulikana hii ni fake.

Wabunifu wengi wana jiuza wenyewe kuliko kuuza bidhaa zao, wengi wanatafuta jina mjini utasikia tu mimi ni “mbunifu wa kimataifa” swali letu ni mbunifu wa kimataifa kwa jina au kwa mavazi unayoyatoa? wengi wanamajina makubwa kuliko kazi zao, ukikutana nae unamjua huyu fulani lakini ukikutana na kazi yake huwezi kuitambua kwa sababu tu ya kuweka mbele wao kujulikana kupata advantages za hapa na pale mitaani kuliko ku-brand bidhaa zao zikajulikana na kukaa kubuni unique things for people to recognize.

Nini mbunifu ana takiwa afanye ili kuacha Legacy katika brand yake kama ataiacha.

Unacho Kibuni Je Kitaishi Miaka Mingine Mingi Ijayo? – Kuacha legacy ni kuwa na uwezo wa kufanya unacho kiacha kiendelee kuishi, kikionwa kina julikana huu ni ubunifu wa fulani, lakini pia je kitatumika miaka hio? Unapo buni kitu unatakiwa kufikiria miaka mingine ijayo sio tu mwaka huo ambao unabuni huitaji mavazi yako yawe Big G ikiisha utamu unaitupa, unahitajika kuwa na mavazi ambayo hata mtoto ambae bado ajazaliwa akija kukikuta aseme yes i can wear this, japo fashion zinaisha ila kuna ile quality na ubunifu wa kitu ambao haupungui hadhi yake. Be neat & creative on your work.

Kuza jina la bidhaa zako kuliko jina lako mwenyewe, kama ukiuliza leo nani ana ana own Gucci watu wanaweza wasimjue, ukiuliza jina la anae own Versace watu hawamjui lakini wanajua kazi zake, wanavaa na kuzipenda na hadi kusema navaa Gucci Original na sio fake kwa sababu tu ya hadhi ya kazi yake. lakini wapo wengi ambao tunawajua majina hapa Nchini kwetu na hatujui kazi zao.

Take risk & don’t follow the rules – fashion ina wigo mpana sana,jaribu kujaribu vitu tofauti tofauti ile mipaka ambayo imewekwa wewe igeuze na kutimia vyema hivyo ndivyo ambavyo wenzetu wanaacha legacy na kuongelewa miaka na miaka.

Don’t follow the trend be the trend setter – unapofuata alicho fanya mwenzio ni wazi kwamba huna uwezo wa kufanya cha kwako, lakini pale ambapo wewe unakianzisha unakuwa mdomoni kwa watu hii fashion umeiona ya sasa? hawa wote wamemuiga fulani yeye ndio alianzisha.

Je unadhani mbunifu gani ana sifa hii hapa kwetu Tanzania kwamba siku asipokuwepo brand yake itaendelea kuwepO?

 

 

Related posts

2 Comments

  1. download video youtube

    … [Trackback]

    […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/je-wabunifu-wetu-wanauwezo-wa-kuacha-legacy-katika-tasnia-ya-mitindo/ […]

  2. click the next page

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/je-wabunifu-wetu-wanauwezo-wa-kuacha-legacy-katika-tasnia-ya-mitindo/ […]

Comments are closed.