Kuchagua jeans ambayo inakufaa ni kazi kubwa hasa kwa wale ambao tuna matumbo/vitambi, wengi wetu huwa tunachagua kuvaa shift dresses au peplum dress kwasababu tu tunahisi haya ndio mavazi pekee yanayotufaa na kuficha vitambi vyetu. Lakini kumbe hata sisi tunaweza kuvaa jeans na tukapendeza endapo tu tutajua ni jeans gani zinatufaa na leo tuko hapa kukupa tips za jeans aina gani za kuvaa endapo una aina hii ya umbile.
- Elewa aina ya umbo lako
Sio kila mwenye kitambi ana umbo la aina moja, kuna wale wanakitambi na apple shape, rectangular shape etc, jua aina ya umbo lako na nini kinakufaa, kama ungependa kujua aina ya umbo lako bonyeza link itakupeleka kwenye series ya aina ya kujua aina ya umbo ulilonalo.
Lengo kubwa kwa wanawake wenye umbo hili ni kupata jeans ambayo itasaidia ku-create a harmonious and balanced silhouette, while emphasizing their best features
Unapoenda kununua jeans zingatia haya
- Comfort
Hakikisha jeans yako haiko too tight wala too loose, hii itakusaidia kuwa comfortable usihisi kubanwa ukashindwa kutembea au kula lakini pia isiwe too loose ikakufanya uonekane mzito zaidi ya vile ulivyo, tafuta jeans zinazo stretchy na ambazo zitakufanya uwe comfortable
- Proportion
Kujua ku-define proportion yako ( usawa wa umbo) ni vyema zaidi, hii inasaidia kukufanya ufiche vile visivyotakiwa na kuonyesha ambavyo unavyo mfano kama unatumbo kubwa unaweza kuvaa high waist jeans ambazo zina balance proportion yako na styles ambazo zinaonyesha ulivyo navyo kama hips & legs.
- Confidence
kitu kingine cha kuzingatia ni kuvaa jeans ambazo upo na confidence nazo, usinunue tu kwasababu ipo kwenye trend au kwasababu imekutosha vyema, tafuta zile ambazo zinanyanyua confidence yako na utajisikia vizuri kuvaa kama jeans ambazo zina built in tummy control.
Elewa Kuhusu Rangi Za Jeans
Kuna rangi mbalimbali za jeans na kuna rangi ambazo zinaweza kukufanya uonekane slim na zingine ambazo zitazidisha kuonyesha umbo lako kwa ukubwa hakikisha unajua rangi gani inakufaa mfano
- Dark Wash Jeans
Hizi ni zile rangi ambazo ni dark mfano nyeusi, dark blue etc, rangi hizi zinazifika kwa kufanya uonekane slim, zinaweza kupunguza muonekano wa tumbo kubwa lakini pia ni rahisi kuzi-style.
- Medium Wash Jeans
Hizi zipo katikati ya dark wash na light wash, hizi hazikufanyi uonekane slim sana kama ambavyo dark zinafanya lakini pia hazionyeshi sana area of concern kama ambavyo light zinaweza kuonyesho hizi zipo 50/50

- Light Wash Jeans
Hizi hazifichi area of concern kama unatumbo kubwa linaweza kuonekana vilevile lilivyo hazina kificho japo unaweza kuzi-style na longer loose top au ukavalia peplum tops.
Elewa Kuhusu Style Za Jeans
Kuna aina mbalimbali za jeans lakini haimaanishi zote zinaweza kuvaliwa na wenye matumbo makubwa kama low rise jeans hizi hazifai maana zinachora tumbo ila unaweza kuvaa jeans za aina hii.
- High Waisted Jeans
Hizi ni nzuri kwa wenye matumbo makubwa maana zinavaliwa juu ya waistline na ku-cover tumbo lako vyema.
- Bootcut Jeans
Hizi ni zile jeans ambazo huwa zinabana juu na kuachia kuanzia kwenye magoti kwenda chini, hizi zinasaidia ku-balance bigger midsection wakati ule mbano wa kwenye hips ukikupa slim effect.

- Wide Leg Jeans
Jeans hizi ni zilepana chini, ukivaa high waist wide leg jeans inasaidia kuondoa attention juu na kuweka attention chini,zinafaa zaidi kama utavalia fitted top ili kuondoa vazi kuonekana too much maana tayari tuna extra details miguuni.
- Straight-Leg Jeans with Stretch
jeans hizi ni zile ambazo upana wa kuanzia kwenye mapaja mpaka chini ni sawa, hazishiki wala kuachia sana chini kitu ambacho kinafanya ziwe comfortable na flattering, chagua ambazo zinavutika ili ku-accommodate tumbo lako na kukupa smooth line.
Namna Ya Kuficha Tumbo Ukiwa Umevalia Jeans
- Muhimu kuchagua jeans ambazo zinasaidia kuficha tumbo lako badala ya kulionyesha zaidi, kama mom jeans,high waistaed jeans etc.
- Complimentary clothing items,
ku-style vazi lako na vitu sahihi ni jambo kubwa zaidi mfano kama unavaa skiny jeans inafaa uvalie lose tops, valia jeans yako na blazer au coat zitasaidia ku-streamline your silhouette, lakini pia kama utavaa darker wash jeans basi valia na ligheter top ku-draw attention juu.
Je Ni Jeans Gani Nzuri Kwa Wenye Vitambi
Kinachofanya jeans kuwa nzuri kwenye aina hii ya miili ni cut na design ya jeans, jeans ambayo ni high rise inasaidia ku-hold tumbo vyema na kutengeneza streamlined silhouette.Na jeans ambazo zina built in tummy control zinasaidia zaidi katika kutengeneza flattering figure
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…