Kama katika pitapita zako ulikutana na kitabu ambacho kilifanya vizuri sana barani kwetu Africa kiitwacho “The Smart Money Women” basi muandishi wa hiki kitabu yupo Nchini Tanzania kutoka Nigeria, Muandishi ARESE UNGWU amekuja Tanzania kutoa darasa maalumu juu ya matumizi ya sahihi ya fedha na namna ya kuondokana na madeni.
Katika kitabu chake cha “The Smart Money Women” Arese ameongelea maisha ya wanadada watano ambao wanamatatizo ya kifedha japo wana kazi nzuri na wanalipwa vizuri ” tunaweza kusema ni kitabu kinacho lenga wadada wengi wa mjini hasa slay queens, japo hata kama sio slay queen unahitaji kujua namna ya kutunza na kutumia fedha zako vizuri
Maisha ya Zuri ambaye ni mhusika mkuu katika kitabu ni mazuri na ameajiriwa katika moja ya kampuni kubwa kabisa Nigeria, analipwa hela nyingi lakini you broke na madeni kibao. Zuri anaamua kukaa na kutafakari anapokosea , anaanza kuandika matumizi ya pesa zake .
Wadada wote katika kitabu ni wa kisasa, wanapenda fashion na kwenda na wakati hivyo walikuwa na matumizi makubwa bila kufuata mpangilio , siku moja Zuri alikaa na wenzake na wote kwa pamoja wakaamua matumizi sahihi ya fedha na wakaamua kuanza matumizi sahihi kwa kufuata budget .
Mwandishi wa ktabu hiki kinachoendelea kufanya vizuri yuko nchini kwa ajili ya darasa huru la wadada juu ya mmatumizi sahihi ya fedha . Event yake itafanyika tarehe 22.06 .2018 saa kumi na moja jioni na utaweza kujipatia kitabu cha bure baada ya kujisajili na kulipia kiingilio. Jisajili sasa kwa linki hii thesmartmoneywomen
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/jifunze-namna-ya-kuwa-muangalifu-na-fedha-zako-kutoka-kwa-muandishi-arese-ungwu/ […]