SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

JINSI MKUFU NA MKANDA UNAVYO BADILISHA MWONEKANO
Mitindo

JINSI MKUFU NA MKANDA UNAVYO BADILISHA MWONEKANO 

48d22bcb97a709222b599a6d17763b9aKatika msimu huu wa ramadhani, vazi lilokubwa na linalovaliwa na wanawake tulio wengi ni baibui, leo nataka tuangalie namna ambavyo tunaweza kuvaa mabaibui yetu kwa kuongezea baadhi ya vikorombwezo ili kulipa mwonekano wa tofauti machoni pa watazamaji wetu.

Baibui si vazi ambalo wengi wanalivaa kwa kuongeza vikolombwezo vingine, lakini nakuhakikishia ukiongeza baadhi ya vikolombwezo ambavyo ntakwenda kuvijadili leo utapata mwonekano wa kipekee na hautapoteza maana ya Stara

Kitu cha kuzingatia kwanza ni kwamba una baibu la aina gani na mtengenezaji wake ameliwekea urembo kiasi gani, ili usipoteze mvuto wa asili wa baibui lako, Hapa namaanisha kwamba unaweza ukawa tayari una baibu ambalo lina urembo wa kutosha hivyo si lazima kuliongezea, unaweza ukaongeza na kulifanya lipoteze mvuto.

Lakini pia unaweza ukawa na baibui ambalo halina urembo kabisa je nini ufanye ili kulitia nakshi?

Moja Unaweza ukavaa Baibui lako na juu ukavalia mkufu , si kweli kwamba ukivaa vazi hili huwezi kuvaa mkufu, ila ni kwamba utawezaje, wengi wetu tumezoea kuvaa mikufu kwa ndani ya blauzi,  Unaweza ukavaa baibu lako kama kawaida na kisha ukavaa mkufu wako kwa nje, hio ndio moja wapo ya kuvaa baibui na mkufu, kama picha hapo juu inavyoonyesha.

Lakini pia unaweza endelea kubadili mwonekano wa baibui lako kwa kuvaa mkanda wa tumboni, na ni vema ukipata mkanda mpana ila si vema ukakubana sana, vingatia hapa unaweza ukavaa mkanda unaofanana na rangi ya viatu au mkoba na hata mtandio

 

Related posts

1 Comment

  1. slot88 online

    … [Trackback]

    […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/jinsi-mkufu-na-makanda-unavyo-badilisha-mwonekano/ […]

Leave a Reply