Jana katika tuzo za malkia wa nguvu 2018 kulikuwa na category mbalimbali ambapo moja wapo ni ya Beauty & Fashion katika upande wa stylist alipewa mwanadada Joujou Styles, Joujou ni moja kati ya stylist wanao fanya vizuri kwa sasa japo kuwa ni upcoming lakini ameonekana kufanya kazi nyingi zaidi kuliko alio wakuta, ame style wasanii mbalimbali kama Vanessa Mdee, Mimi Mars, Ben Paul na wengine wengi.
kutokana na udogo wake katika hii Tasnia likatujia swali Je Joujou amependelewa hii tuzo au ana stahili? tukiangalia kuna watu wengi wambao wamekuwa wakijaribu ku-push katika hii Tasnia ya mitindo kuna mwanamama Khadija Mboka, Asya Khamsin, kuna stylist kama Swalha Msabaha, fashion bloggers kama Shamim Mwasha wa 8020 na Mariam Ndaba wa Missie Popular hawa ni watu ambao wengi tuna look up to katika mitindo lakini tuzo hii ikamuangukia Joujou.
Hatusemi kwa ubaya Joujou she real is pushing, mchango wake unaonekana hasa katika video za wanamuziki sasa hivi video nyingi ame zi style yeye na nyingi tunazipenda mionekano yake mizuri ana badilika na anampa mtu muonekano unaoendana nae, tunadhani hii iwape motisha wengine ya kujaribu kufanya kazi kwa nguvu zote Joujou japo na udogo wake amepata Tuzo hii kubwa ya heshima na ni mara ya kwanza hiki kipengele kuwepo katika Tuzo hizi.
Anajitahidi sana kufanya kazi na watu mbalimbali bila ya kujali udogo wake she shoot her shot na mwishoe effort zake zimeonekana, tukiangalia kwa mwaka jana na mwaka huu wasanii wengi wamekuwa styled na yeye. kwetu sisi tunaona she deserve a tuzo kama waliangalia stylist aliye fanya vizuri mwaka jana na mwaka huu.
Je wewe kwako unaonaje? well deserved au kapendelewa?
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/joujou-styles-na-tuzo-ya-beauty-fashion-je-amependelewa-au-anastahili/ […]