SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jua Namna Ya Kuondoa Harufu Mbaya Ya Viatu
Dondoo

Jua Namna Ya Kuondoa Harufu Mbaya Ya Viatu 

Hivi Ushawahi kuwa kwenye Mkusanyiko wa watu na Mara ghafla waanza kusikia Harufu mbaya na Hapo Hapo unabaini inatoka kwenye viatu. Utajisemesha Nani huyo kuvua viatu? Huku ukibana pua. 
Kama hujawahi kukutwa na jambo hili huwezi kuelewa vile mhanga anavyojisikia. Baada ya kumaliza kusoma hapa hutotaka tena ukumbwe na shida hii 


VIATU KUTOA HARUFU MBAYA 
Hali ya viatu kutoa harufu mbaya inawezekana ilishawahi kukukumba ama bado inakukumba au ushawahi kukarahishwa na mtu mwenye tatizo hilo ,leo nitaeleza mambo ya kufanya ili uondokane na tatizo hilo ambalo husababisha watu kutojiamini pindi wanaopokua katika kundi la watu.

 • Vaa viatu vinavyokutosha usivae viatu vinavyokubana, Kwa sababu unapovaa viatu vya kubana husababisha viatu kutoa jasho jingi ambalo hupelekea ukuaji wa bacteria na fungus wanaotoa harufu.
 • Vaa viatu ambavyo vinaweza kupitisha hewa mfano viatu vya ngozi,nk
 • Badilisha viatu :Usivae viatu pea moja kila siku. Ili kuvipa nafasi vile vingine. Kama huna vingine Fanya usafi wa viatu vyako na soksi kila siku. 
 • Wakati wa usiku(au kama kuna kiubaridi usiku viache viatu nje halafu asubuh vianike )kwa kufanya hivyo huweza kuwapunguza bacteria wasababishao harufu mbaya
 • . Usirudie soksi. Kufanya hivyo unaita fungus wanaoweza kusababisha  harufu mbaya. 
 • Osha miguu yako kila siku kwa sabuni.
 • Vioshe viatu  angalau mara 1 kwa wiki.( Uzingatie na malighafi ya viatu husika ili usiviharibu) 
 • Vaa soksi pindi unapovaa viatu.
 • Tumia majani ya chai kutoa harufu mbaya ya viatu. Paketi moja inatosha unaniacha kwenye kiatu inaweza kutoa harufu mbaya yote. 
 • Pia kuna Feet up spray zinapatikana sehemu mbalimbali maalum kupuliza kwenye viatu vyako ili visitoe Harufu mbaya. Harufu inatoka nzuri na utajiamini hasa! Zitumie 
 • Vaa viatu kuendana na muongo wa Hali ya hewa na sehemu unavyokwenda. Mfano Wakati wa jua Kali sio Wakati wa kuvaa viatu vyenye malighafi nzito nzito joto linavutia fungus wanaoweza kusababisha harufu mbaya na ya ajabu. 

Jee unajiamini kuvua viatu vyako mbele za watu kila inapobidi au una hofu? 

©binturembo 

Related posts