Hatudhani kama inabidi kilakitu kinahitaji kuongelewa kwa Tasnia ya urembo na mitindo Tanzania ndio tuamke na kuanza kuyafanyia kazi, ilikuwa kilio cha wabunifu na wanamitindo kwa wasanii kuwatumia katika kazi zao. Kilio kimesikika na sasa tunaona kwenye video music za Tanzania wanamuziki wanatumia mavazi ya wabunifu pamoja na wana-mitindo kutoka Tanzania.
Kwa sasa ukiangalia video nyingi wasanii au wanamitindo wanavalishwa mavazi kutoka katika collection za wabunifu kutoka Tanzania, mfano mzuri ni video ya The One kutoka kwa Diamond Platnumz, ambapo unaweza kuona mavazi ya models yametoka katika collection ya mbunifu
Tofauti na ambavyo tulitegemea kwamba mbunifu ataona hio fursa na kutangaza kwamba ni kazi yake, hakuna siku hata moja tumeona mbunifu huyo akipost kusema kwamba ile ni kazi yake. Wimbo una trend number moja youtube, umeangaliwa na mamilioni ya watu ambao wanatoka sehemu mbalimbali na bado mbunifu hajaichukulia hii kama fursa katika biashara yake. Na hii sio kwa huyu tu mmoja bali ni wengi ambao wanawavalisha wasanii mbalimbali bila kuji-credit kazi zao.
Lakini pia wanamitindo wanapewa fursa kuonekana katika videos hizi na wao pia hawaoni kama hii ni fursa katika career zao na kujitangaza. Nani hatotaka kufanya kazi na wewe kama umeonekana kwenye video ya mwanamuziki mkubwa? kuanzania agencies mpaka makampuni mbalimbali?
Tunahitaji kujifunza zaidi kujitangaza katika biashara zetu, kila kitu kinachotokea ni opportunity ya wewe kupiga hatua mpya.
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/kunauhitaji-wa-elimu-ya-biashara-kwa-wabunifu-na-wanamitindo-wa-tanzania/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/mitindo/kunauhitaji-wa-elimu-ya-biashara-kwa-wabunifu-na-wanamitindo-wa-tanzania/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/kunauhitaji-wa-elimu-ya-biashara-kwa-wabunifu-na-wanamitindo-wa-tanzania/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/kunauhitaji-wa-elimu-ya-biashara-kwa-wabunifu-na-wanamitindo-wa-tanzania/ […]