SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Kwanini Hupaswi Kukosa Kuwa Na Viatu Aina Ya Boot Na Jinsi Ya Kuvistyle Katika Hali Ya Hewa Ya Joto
Mitindo

Kwanini Hupaswi Kukosa Kuwa Na Viatu Aina Ya Boot Na Jinsi Ya Kuvistyle Katika Hali Ya Hewa Ya Joto 

Katika aina ya viatu tisa ambavyo hupaswi kukosa kuwa navyo kimoja wapo ni viatu aina ya boots, ni muhimu sana kuwa navyo hasa katika majira ya mvua na baridi, lakini hivi viatu sio tu kwa ajili ya mvua na baridi vinaweza kuvaliwa hata msimu wa joto na vipo very fashionable na stylish. Kwa bahati mbaya ni mara chache sana utakuta mtu amevaa boots katika maisha ya kawaida na hii ni kutokana na kuamini kwamba viatu hivi ni vya msimu wa mvua na huku kwetu sisi ni joto.

Kwanini Hupaswi Kukosa Kuwa Na Viatu Aina Ya Boot?

 • Fashion – boots ziko very fashionable na kwa sababu sio wengi hupenda kuvaa, mtu anapovivaa anaonekana wa tofauti.
 • Unaweza Kuvitumia Mara Nyingi – Boots ni moja ya viatu ambavyo unaweza kuvaa mara nyingi na mavazi aina tofauti, kuanzia suruali, short pants, gauni na hata skirt inategemea na mapenzi yako ya nini ungependa kuvalia siku hio
 • All Year Around – Kama ambavyo tulisema mwanzo boots zinaweza kuvaliwa wakati wowote wa msimu, baridi,joto,mvua, kipupwe zenyewe zinavalika inategemea na wewe unavyo style, kama kuna joto basi inabidi uvalie mavazi ambayo sio mazito, kama baridi unavalia mavazi mazito na same kwa misimu mingine.
 • Zinavaliwa Kokote – Yes kuanzia red carpet, casual, unaweza kuzivaa hata ofisini pia as huwa tunasema kila siku kila kitu kinategemea na jinsi ambavyo una style kufika sehemu ambayo unaenda, sawasawa na boots.

Jinsi Ya Kuvistyle Katika Hali Ya Hewa Ya Joto

 • Vaa na mavazi mwepesi

Boots zinaweza kuwa na joto miguuni, ili kupata uwiano na kutokuleta joto juu ya joto tunashauri uvae boots zako na mavazi mwepesi ili kupata uwiano na hewa.

 • Colorful

Jaribu kuvaa boots zako na mavazi yenye rangi kama nyeupe au rangi yoyote lakini si nyeusi kama ambavyo tunajua rangi nyeusi husharabu mwanga na kuleta joto wakati rangi nyingine huakisi mwanga wa jua.

 • Valia Mavazi Mafupi

Vaa boots zako na mavazi mafupi kama t-shirt dress, short dress, short pants au skirt ilikuupa mwili hewa na kupata hewa miguuni pia kama utataka kuvaa na mavazi marefu hakikisha kitambaa chake ni chepesi.

 • Chagua Boots Zanye Rangi

Summer is colorful, sio lazima boots zako ziwe nyeusi unaweza kuchagua rangi nyingine kama pink, nyekundu etc, lakini pia unaweza kuchagua boots zenye kitambaa chepesi na sio zile nzito za baridi.

Kama wewe ni boot lover lakini ulikuwa unafikiria utavaaje boots kipindi cha joto ni matumaini yetu tumekusaidia, lakini pia kama hukuwa unapenda na ungependa kujaribu baada ya kusoma hii article usisahau kupiga picha vazi lako na kututumia picha yako katika mitandaoย  yetu ya kijamii

Related posts

1 Comment

 1. rich89bet

  … [Trackback]

  […] Here you can find 1675 additional Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-hupaswi-kukosa-kuwa-na-viatu-aina-ya-boot-na-jinsi-ya-kuvistyle-katika-hali-ya-hewa-ya-joto/ […]

Comments are closed.