SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Kwanini Ni Muhimu Kuwa Na Style Yako
Mitindo

Kwanini Ni Muhimu Kuwa Na Style Yako 

Kama kuna kitu ambacho tume-notice ni kuwa wengi wetu kwa sasa hivi tunamionekano sawa, wengi kila mmoja anaonekana sawa na mwingine na hii inatokana na wengi wetu kutokujua kuhusu style zetu au ku-copy style za wengine mpaka tunasahau ni nini sisi na mioyo yetu tunataka.

Ukiangalia kwa wenzetu hasa watu maarufu utagundua kwamba wengi wanajitahidi kujiweka tofauti na wengine kila mtu anamuonekano wake ambao unajua kabisa fulani hii ndio style yake na ni tofauti na fulani. Mfano mzuri ni Rihanna, Beyonce, Kim Kardashian, na wengineo japo hapa kwetu pia wapo wachache kama Juma Jux, Ally Rehmtullah, Salama Jabir, Ali Kiba, Mbosso, Vanessa Mdee Etc. Hawa ni wale ambao wanamionekano fulani ambayo ni tofauti na wengine iwe ni crazy au calm style.

  • Personal Style Ni Nini?

Ni mtindo wako, ni namna ambavyo ungependa muonekano wako uku-represent vile ambavyo wewe unahisi unataka au ungependa kuonekana. Mtindo wako unaweza kuonyesha kile unacho kisimamia, Unaweza kukufanya uonekane wa kipekee kama utataka kuwa wa kipekee lakini unaweza kutumia muonekano wako kama zana ya kujulikana na kutambuliwa na kujiimarisha kama mtu wa kitaalam ( professional)

  • Now Kwanini Kuwa Na Personal Style Ni Muhimu Kwa Brand Au Mtu Wa Kawaida
  • Style Yako inakutofautisha na wengine

Yes, style inaweza kukufanya u-stand out na kuonekana wa kipekee katika group la watu wengine, mfano mzuri ni Rihanna kwa sasa anajulikana kwa kuvaa mavazi ambayo wengine tunaweza kuyaona ni ugly lakini yeye anauwezo ya kuyafanya yaonekane mazuri na hapa sio kwamba kwa sababu mavazi hayo sio mabaya hapana bali ni namna ambavyo anaya-style.

  • Kukufanya uwe memorable

Ukiambiwa leo Michael Jackson atakumbukwa kwanini kutokana na mavazi yake then utasema hats, gloves, jackets etc lakini pia tunamjua Mrisho Mpoto kwa kutembea peku, tunamjua Salama Jabir na tomboy style zake hapa kwetu Tanzania ambapo ni moja kati ya watu maarufu wachache wenye style hii.

  • Confidence

Unapovaa kitu ambacho ni style yako unajisikia vyema unahisi umependa na unakuwa true to yourself, Mfano unatakiwa kwenda ofisi fulani kwa ajili ya kutafuta ajira basi utajaribu kutafuta mionekano inayoendana na sehemu hio hii haikatazwi ila tu kama utafanya muonekano huo uendane na style yako, lakini kama wewe ni mtu wa skirt ndefu lakini ukaona hio sehemu wanavaa skirt fupi na wewe ukaamua ku-copy ili kuendana nayo lazima utakosa confidence lakini kumbe ungevaa kile ambacho wewe unakipenda ungejiamini na kuweza kufanya interview yako vyema.

Well hizo ni sababu tatu kwanini personal style ni muhimu, unaweza ku-share na sisi sababu nyingine ambazo unaona kuwa na style yako ni vyema hapo chini katika box letu la comment.

Related posts