Tukiwa tunaingalia Tasnia ya mitindo na urembo unaweza kuona wanamitindo (models) wana play part kubwa sana kukuza Tasnia yetu hii, Wabunifu wanawatumia wao kutangaza kazi zao, makeup artist vile vile, hair stylist pia, wanamuziki wanawatumia haohao models lakini kwa bahati mbaya ndio watu ambao hawana maendeleo katika Tasnia hii, Hii imetufanya kujiuliza kwanini wanamitindo wanakuwa masikini?
Ukiangalia wengi ambao tunawaona wameendelea na wana afadhali ni wale ambao wametoka Nje ya Nchi au wale ambao wameamua kujitafutia maisha yao kivingine na kufanya modelling kama hobby wale ambao wanasubiri kupanda katika jukwaa ndio wapate pesa wengi wao wanaishia kupata majina na mwishoe wana give up na tasnia na kwenda kufanya jambo lingine, tofauti na wenzetu ambao wao Modelling ni kama kazi inawalipa. Tumeona mwaka huu mwanamitindo Kendall Jenner ametajwa kuwa ndio model anaelipwa zaidi kupitia her modelling career tu bila ya biashara nyingine je sisi tunalipa models?
Kusema ukweli sisi akija mtu akasema anataka kuwa models lazima tutamwambia usitegemee hii kuwa kazi kwa maana hailipi ukiachana na kupata jina na followers Instagram hakuna ambacho utapata modelling tunaweza kuiita hip hop ya Tanzania career ambayo “HAILIPI” watakutumia kwenye video’s, runway’s zao watakutumia katika matangazo yao na kukulipa kiasi kidogo kama sio kufanya bure kabisa kwa kisingizio cha kukupa jina, wakisahau kwamba unaweza kumtafuta yoyote ukafanya nae umpe hilo jina lakini mpaka umekuja kwangu ni kwamba umeona cha tofauti na unahitaji kulipia utofauti wangu. Tasnia ina kuza wanamitindo masikini.
Opportunities chache kama kuna watu ambao wana opportunity chache ya kazi zao ni models, hakuna hafla nyingi za mitindo zinazo fanyika Nchini na hata zikifanyika wanahitajika wachache katika mia wanaweza kuchukuliwa kumi au watano na kuwaacha wengine wakiendelea kusota kusubiri nafasi katika show nyingine. Lakini pia kazi kama kuonekana katika music videos wanamuziki wengi wanaenda kufanyia video’s zao nje na kuwaacha models wa ndani, hii inapelekea models wa ndani kukosa nafasi za kazi hata katika zile chache zilizopo zinapelekwa Nje.
Kufuata Jina kama huna jina, kama huna followers utasota sana katika modelling kwa maana wanao chukuliwa ni wale wale ukiangalia katika runways sura zilezile, ukiangalia music videos walewale ukiangalia matangazo wale wale wengine wanabakishwa na hata ukiwa na jina ni vile tu unataka kuonekana bado upo hata kama haulipwi utafanya tu ili jina lako lisi-fade away.
Kutokuwa na mikataba mizuri na modelling agents, Agents wanaweza kukufanya ufanikiwe au kukunyonya kama wewe ni model ambae upo chini ya agent fulani hakikisha mkataba wako uko salama na ni fair kwako na wao, Agents nyingi zina nyonya ma-models, get yourself a lawyer akueleweshe kipengele hadi kipengele na uone kama mkataba unakufaa au hapana kabla ya kusaini na kuingia mkataba na agent hizo.
Well broke models wanatengenezwa na Industry kwa maana hawachukuliwi serious na industry kama wangekuwa wanapewa kipaumbele basi wengi wao sasa hivi wangekuwa mbali, kuwa katika Tasnia ni jambo moja wakati tuna process Tasnia ikuwe lakini pia tungependa waliopo kwenye Tasnia nao wawe na madiliko katika vipato vyao.
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-tunakuza-wanamitindo-masikini/ […]