SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Kwanini Tunanunua Nguo Na Kuishia Na Mavazi Tusiyoyapenda?
Mitindo

Kwanini Tunanunua Nguo Na Kuishia Na Mavazi Tusiyoyapenda? 

Umeshawahi Kujiuliza Kwanini Ni Wewe Mwenyewe Unaenda Madukani Kununua Nguo Kisha Unakuwa Na Kabati Lina Mavazi Mengi Na Huyapendi? Inashangaza Right? Well Hii Hutakona Na Kwamba

  • Unanunua Vitu Vilivyo Kwende Trend Kwa Wakati Fulani

Wengi huwa hatununui mavazi ambayo ni timeless tunaangalia nini kina trend kwa wakati huo na ndio hichohicho tunanunua na kuvaa mwisho wa siku trend inaisha tunabakia kuwa na mavazi mengi kabatini ambayo hatuyavai na hatuyapendi tena.

  • Unanunua Kwasababu Umemuona Fulani Kavaa Na Kapendeza

Unaweza kumuona mtu maarufu au jirani yako kavaa vazi akapendeza na wewe ukaenda kununua kama hilo, mwisho wake unalivaa mara chache na kuona halifai tena unaliacha na kurukia vazi lingine. Lakini kumbe ukikaa ukajisikiliza na kujua wewe binafsi unapenda mavazi ya aina gani basi ungekua na kabati limejaa mavazi uyapendayo.

  • Unanunua Ukidhani Utapungua Au Utanenepa Na Zitakutosha

Wangapi tupo guilty na hili? lol unanunua vazi kwasababu tu umeanza diet au gym ukijua utakonda au kwasababu umeanza kula unajua utanenepa unanunua vazi ili ukipungua au ukanenepa ulivae mwisho wa siku mwili unakugomea unabaki kuliangalia tu lile vazi kabatini na misonyo ya kujilaumu kwanini umenunua. Instead nunua mavazi kutokana na hali uliyonayo wakati huo incase ukinenepa au kupungua utafanya shopping upya.

  • Unanunua Bila Kupangilia Au Kufikiria Kuhusu Vile Ulivyonavyo Tayari

Unaweza kujikuta na mavazi aina moja yamejirudia mara nyingi kabati kwako au ukaijikuta vazi fulani linaendana na nguo fulani tu huwezi kuvaa na nyingine hii ni kwasababu hatufikirii vile vilivyopo tayari, mfano ukinunua shirt waza utalivaa na suruali gani kabatini kwako na je kuna vazi lingine ambalo utaweza kuvalia hio shirt tena?

Makabati Yetu Yanapaswa Ku-reflect Maisha Yetu Inatakiwa Tujisikie Vizuri Tunapovaa

Related posts

1 Comment

  1. purple mystic mushroom vs golden teacher,

    … [Trackback]

    […] There you will find 87930 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-tunanunua-nguo-na-kuishia-na-mavazi-tusiyoyapenda/ […]

Comments are closed.