Tunadhani since tumeanza blog na wale tulio wakuta kuna models wachache sana ambao wanasikika au wanaandikwa International hawa ni wale ambao waliwahi kuwa Ma Miss eidha miss Tanzania au Miss Universe, kuna watu kama Hapiness Magesse, Tausi Likokola, Miriam Odemba na Herieth Paul hawa wote wanatuwakilisha vyema huko Duniani lakini ni kwanini wao kila siku? Kwanini wengine hawatokei wa miaka hii? nini kibaya? Tumekuja Kugundua
Kama Kuna Kitu Miriam Odemba,Happiness Magese, Herieth Paul wanacho in common ni determination ya kupata kile wanacho kitaka kitu ambacho most of our models sasa hivi hawana, Models wengi wanalalamikia agency,wanalalamika tasnia ya mitindo haichukuliwi serious lakini wao wenyewe pia hakuna wanacho Fanya kuonyesha wanataka kukua.
Models ni wengi mno kwa sasa na kuna vitu vingi wanafanana hawana uniqueness wengi hata pose za picha hawazijui model anapiga picha ya portfolio Kama anapiga selfie ya kuweka profile picture Whats App na wengine hata hawajui tofauti ya modelling na video vixen wote wana vichanganya pamoja, hii inapelekea kuwa na utitiri wengi wa models ambao hawana quality ya kuwa models.
Mitandao ya kijamii
these days kila mtu anaweza kuwa model, ukiwa maarufu basi wabunifu watakukimbilia kufanya na wewe kazi kisa tu unajina au followers zaidi ya laki moja ambao yeye akikuvalisha wataona na kunununua, kuna ambao wanafanikiwa na hii mbinu na kuna ambao wana angukia pua kwa maana anaweza akawa amebuni mavazi mazuri lakini kutokana na mtu aliye mvisha kutokujua afanye nini basi kinacho tokea hapo ni kichekesho.
Tukiongelea kuhusu catwalk katika runway ndio kabisa na wengine wapo kwenye tasnia miaka mingi lakini bado wanatembea mbaya that makes us wonder nani atakuchukua katika agency yake ufanye nae kazi Kama miaka yote hio hujajifunza kutembea? who would want mtu ambae anatembea kwenye run way za wabunifu wakubwa akiwa hajajifunza kutembea? we need to take time and teach these people such things, how to walk, how to pose etc.
https://www.instagram.com/p/BeiQNsEgSAs/?taken-by=heriethpaul
Mazoezi
Models wengi wa sasa hawana mazoezi wakisha panda katika majukwaa ya Fashion mara mbili tatu wana jikuta wamemaliza wanajua kila kitu, kitu ambacho si kweli practice makes it perfect hii ndio hupelekea unapo rudi katika run way tena na tena unaonekana up coming,practise kila siku. Tembea hata nyumbani chukua simu weka pose jipige angalia angle yako nzuri ni ipi, jifunze kuwa na nyuso tofauti we can swear models wa siku hizi wana nyuso sawa za kupakwa makeup, hawana the fierce model look ni wamepoa tu kama maji ya mtungi.
Kuridhika
Wengi wana ridhika na kuitwa model mkubwa wa Tanzania, kuitwa hivyo haimaanishi umesha maliza Duniani, kama una taka kweli kufika International unapo fikia ngazi ya Nchi hio ndio nafasi nzuri ya wewe kutumia ulicho nacho kufika mbali zaidi, watu wakuone kila siku unatamani kufika mbali make your goals for people to see, sio tu kwa kuongea bali efforts pia, have your unique looks, walk, personality etc. be professional models wengi kwa sasa wana lack professionalism, wana piga picha za ajabu na kila siku mitandaoni kujibishana na watu. Hapo ndipo ambapo watu wanaanza kukuchukulia kawaida na kukuona mwenzao.
Well soon tutawaletea nini ufanye kufika international na njia zipi upitie kwa hapa Tanzania kufika mbali, stay tune & make sure kuwa unapitia pitia hapa.
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-tunasikia-international-models-wale-wale-kila-mwaka/ […]
… [Trackback]
[…] Here you can find 9449 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-tunasikia-international-models-wale-wale-kila-mwaka/ […]
… [Trackback]
[…] There you can find 69692 more Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-tunasikia-international-models-wale-wale-kila-mwaka/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-tunasikia-international-models-wale-wale-kila-mwaka/ […]