Ukipata nafasi ya kuitwa kwenye interview, nina uhakika utahakikisha kila kitu kuhusu muonekano wako kiko sawa kwanzia kwenye nywele, makeup, mavazi, viatu, harufu na usafi kiujumla. Hii ni kwasababu unafahamu bila shaka kuwa muonekano wako ni sehemu ya CV yako.
Mwajiri hatazami tu vyeti vyako wala kile unachokisema tu bali pia unavyoonekana. Kama ilivyo katika interview, muonekano ulionao ni CV yako katika maisha halisi. Mtu anapokutana na wewe kwa mara ya kwanza, hatazami kilichopo moyoni. Like for real..macho ya binadamu sio scanning machine ya utu wa mtu so mtu anapokuona kwa mara ya kwanza anahukumu wewe, tabia zako na utu wako kutokana na muonekano wako.
Katika muonekano kuna mengi, twende taratibu kwanzia kichwani mpaka miguuni. Mtu anapokutazama anakutafakari kwanzia katika style ya nywele uliyoiweka na unadhifu wa style hiyo, nguo ulizovaa, mtindo wa hizo nguo na namna zinavyokustiri, anatazama viatu ulivyovaa, mkoba au begi lako, makeup uliyopaka yani kama inaendana na mazingira na ilivyokukaa na pia namna unavyojibeba. So hapa tunaona kuwa sifa ya kwanza ya muonekano ni kuwa CV.

Muonekano sahihi unakufanya ujiamini, ujipende zaidi na huboost mood. Kuna kijifeeling fulani so positive unapopendeza, you just feel happy inside, mtu akikusifia ndio kabisaaa! When you look good na unajua you look good you feel positive na unapata uchangamfu. Mood yako inakuwa nzuri na hii inasaidia kufanya kazi na maamuzi kwa ufasaha. Akili hujua kabisa unapopendeza na hii hufanya upate ujasiri zaidi. Muonekano mbaya huondoa ujasiri. Nikukunbushe tu, look better…not Perfect! But if you can look perfect, please do but unatakiwa uweke juhudi katika kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa

Muonekano wako unavutia watu sahihi maishani mwako. Kila mtu anapenda kujihusisha na watu wa maana wanaoendana na Imani, misimamo na ndoto zake, hapa naongelea marafiki, business partners nawapenzi. How you look inamwambia mtu either njoo jihusishe na mimi au kaa mbali na mimi. Kila mtu ana uhuru wa kuchagua muonekano lakini ni muhimu kuhakikisha unakuwa na muonekano unaotuma ujumbe unao utaka kukuhusu.

Lets assume Sara ni binti mjasiriamali amefungua kampuni yake ya kusambaza chakula cha diet maofisini. Sara yuko katika hatua za kutafuta wateja katika ofisi mbalimbali. Sara anajipenda sana hivyo asubuhi hiyo anaamka na kujiandaa. Kavaa top inayoonyesha bra kwa ndani na mini skirt ya jeans fupi sana simple nyekundu kumatch na handbag yake, ana kiduku kichwani kinacho endana na sura yake. Sara ni mpishi mzuri sana na anajua vitu vingi kuhusu diet
Anapo ingia ofisi ya kwanza anakutana na binti mwingine anayetafuta wateja wa juice asili. Mwenzake kavaa jeans na shati ya mikono mirefu ya chiffon nzito aliyochomekea ndani ya jeans yake. Kaweka mkanda mweusi juu ya jeans na simple kukamilisha muonekano wake. Unadhani kati ya hawa mabinti wawili nani atapewa nafasi ya kuongea na utawala? Wote wamependeza na ni nadhifu, wote wana idea nzuri na wote wanatafuta ridhiki lakini watu hawata tizama nia yako kwanza wala tabia yako bali namna ambavyo ulivyoji – present. Katika hili unaona kuna umuhimu wa kuzingatia tu si uzuri wa muonekano wako bali pia kama muonekano wako ni sahihi kwa mazingira uliopo.

Tupo katika ulimwengu unao sisitiza kujikubali ,Wenyewe wanasema BE YOURSELF. This is good na n ijambo la msingi lakini nadhani watu wengi wanatafsiri hili neno vibaya. Usitegemee kuwa rough then upate a smart gentleman as your boyfriend kirahisirahisi tu, Unataka kupandishwa cheo lakini kujijali wewe na muonekano wako tu ni issue, unatamani kuchukuliwa kama kiongozi lakini unavaa mavazi ya kukuexpose sana maumbile. Ndoto zako na malengo yanapaswa kuendana na muoneka no wako
I don’t mean uvae ujifunike hadi miguuni but I mean dress appropriately…kama ni model then dress the part, stylist dress the part, mdada katika sekta maalum basi vaa unavyotakiwa, kwenda katika first date vaa how you want huyo mwanaume akuaddress. Take care of your body kwanzia katika afya hadi mavazi. Kama una- any excuse katika hili I have bad news for you, YOU ARE LAZY AU YOUR MENTALITY NEEDS SOME WORK. If you expect better things maishani, ni lazima uwe bora kwanza. You want a better job, a better man, more respect, kupandishwa cheo, kupata fursa mbalimbali, kupewa nafasi za uongozi…You have to look the part. Hakikisha muonekano wako una endana na malengo kwasababu hii inaongeza nafasi ya wewe kuyafikia.
Imeandkwa na @elegancebyRee
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-uboreshe-muonekano-wako/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-uboreshe-muonekano-wako/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-uboreshe-muonekano-wako/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-uboreshe-muonekano-wako/ […]