Collection yake ya kwanza ilikuwa katika stara fashion week 2018, lets say hana hata mwaka katika game ya mitindo na tayari tumeshaona effort zake kiasi ambacho tukaamua kukaa chini na kuandika kuhusu yeye. Kama ni mara yako ya kwanza kulisikia hili jina anaitwa Irada Mahadhi Au @Iradastyleofficial kama ambavyo anavyojulikana katika mitandao ya kijamii ni moja kati ya wabunifu wazuri kabisa wa mavazi ya stara lakini hachagui hata kama sio stara yeye anakubunia, ni hijab stylist pia. Kwanini tumesema wabunifu wamuige Irada Style.
- Anafikiri Kama Mjasiriamali
Tip namba moja katika ku-make it kwenye fashion business ni kufikiri kama an entrepreneur, achana na kwamba mimi nina jina watu watakuja fikiri kama mmachinga kila siku nadi kazi yako, na hicho ndicho akifanyacho Irada ukipita katika page yake hapitishi siku bila kupost kazi yake iwe amevaa mwenyewe au amevalisha mtu.
- Wekeza Katika Kazi Yako
Ubunifu ni kazi kama kazi nyingine as inakuingizia hela, Irada ana wekeza kuanzia katika material anayo tengenezea mavazi haya, tumesha zoea kuona prints zilezile katika majukwaa ya mitindo lakini ukiingia katika page ya Irada utakuta vitu tofauti material ya tofauti na quality, lakini pia tumezoa kuona wabunifu wakisubiri fashion show fulani ndio watoe collection zao mpya labda wakihofia kutumia pesa sana kwa Irada ni tofauti anatoa collection zake mara kwa mara lakini pia juzi tu ametoka kufanya Pop Up Shop ya kwake mwenyewe. That Is What We Call An Investment.
- Bei
Kingine tunacho penda kuhusu Irada tofauti na wabunifu wengine mpaka umfuate personal kujua bei yeye huwa anataja bei katika page yake mtu anajua kabisa akitaka hili vazi anapata kwa kiasi gani lakini tulisha wahi kuongea nae kuhusu bei wengi wanalalamika ni kubwa akasema ni material anayo nunua lakini mtu akitaka kwa cheap inawezekana ila sio kwa same material ( its called knowing your customer and satisfying them)
- Social Media Best Friend
Irada ana tumia sana kutangaza kazi zake kupitia social media ambapo kwa sasa biashara zinafanyika sana huko, kuna wabunifu unaweza kujiuliza bado wapo? kweli bado wanabuni? page zao zimejaa sura zao na bata zao tofauti na Irada huwa anapiga quality pictures akiwa amevaa mavazi yake kuvutia wateja.
- Do It Right
Kuna trend ya wabunifu kuchukua models ambao wana kiki mbaya ili kukuza jina, au kutangaza kazi zao katika page za udaku kuna msemo wa waswahili husema “kizuri kinajiuza kibaya cha jitembeza” utamvalisha model ataongelewa halafu itaisha then? what next? Je watu ambao hawapendi hayo maswala watakuja kuvalishwa na brand yako? unajua target yako? wakati Irada yeye anatumia model wowote na kumvalisha kazi zake huku akim-style vyema kabisa ku-catch people’s attention.
Kama wabunifu wa zamani au wewe ni mpya jifunze hivi vitu na uangalie ambavyo game yako katika kupata wateja itabadilika, jua nini unataka na invest katika hiko kitu usitake jina la haraka la kukurupuka ndio maana wengi wana fail, take baby steps lakini ambazo zinamanufaa kwako, Irada anatoa collection mara kwa mara akagundua anahitaji afanye kitu apate kupunguza mzigo aingize mwingine amefanya pop up shop na sale kwa pamoja ( entrepreneur mind) huku aki-introduce collection yake mpya ya eid kaalika watu mbalimbali katika sekta ya mitindo na habari, habari zake zimewafikia watu wengi kwa just one simple act.
Related posts
5 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-wabunifu-wamuige-irada-style/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-wabunifu-wamuige-irada-style/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-wabunifu-wamuige-irada-style/ […]
… [Trackback]
[…] There you will find 37295 more Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-wabunifu-wamuige-irada-style/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/kwanini-wabunifu-wamuige-irada-style/ […]