Hutakiwa kumaliza hela za kwenye kibubu chako ili upendeze, kuna namna mbalimbali za kukufanya wewe uonekano Bad & Boujee in cheap thrills outfit, mwandishi wetu @raymimie anakujuza zaidi hapo chini
Zingatia ubora wa kitambaa
Nalisisitizia hili kwasababu sisi ni wanunuaji sana wa nguo za mitumba. Nguo kadhaa za mtumba huwa zimechuja rangi au kunyonyoka nyuzi. Ubora wa kitambaa huchangia sana kwenye muonekano wako. Kitambaa kizuri kitafanya uonekane ghari wakati nguo yenye kitambaa kichovu itafanya uonekane cheap. Bila kujali bei kuna material huonekana za bei chee, hata kama ukweli ni kwamba inagharimu mfano ni baadhi ya satin, zaidi ikiwa imeshonwa vibaya.
Rangi ni kitu muhimu, zipangilie
Kuna rangi zinafanya mtu afifie na nyingine hufanya mtu apop. Vaa rangi zinazovutia na kukung’arisha. Achana na nguo zenye rangi zilizofubaa zitafanya uonekane umechoka na kuchakaa. Tumia vitu vya gold, isiwe ile gold ambayo hata kwa mbali unaona ni fake. Yani gold kama heleni za chinga. Gold hunogesha nguo sana. Unaweza vaa kwenye accessories au kwenye nguo ila isiwe nyingi sana labda kwa usiku.
Chomekea
Kuna kitu kuhusu kuchomekea kinachoongeza unadhifu. Unaonekana smart na ghafla muoneka wako unahama kutoka kuonekana kama mtu asiyejal na kuwa mtu aliyekuwa put together. Kuchomekea pia hufanya uonekane more formal.
Vaa statement accessories
Sasa badala ya kununua na kuvaa accessories nyingi kwenye vazi moja jitahidi kununua kuvaa chache sana zinazovutia na kumuacha mtu akitafakari. Vaa hereni kubwa zenye mtindo wa kipekee au hereni ndogo sana na cheni pana. Tassel na button earrings ni nzuri sana na huongeza unadhifu wa mavazi. Vaa mkanda unaostand out au/na bold lipstick au vaa pochi inayokaa. Take risks baby girl..ndio mitindo yenyewe ila usiweke vitu vingi kama umepania. Imagine kichwani berret, kiunoni zile bags za kiunoni na offwhite belt hapohapo, chini grandma shoes…too much, not good, please change, hutembei na mimi.
Wekeza kwenye coats, blazers,pointy shoes
Kuna mavazi uwa ni classical, yani zungukaa ila vitakuepo. Nunua point shoes, nunua vifupi virefu na flat. Sasa hivi kuna pointy sandals pia. Pia nunua koti, leather, oversize coats, na blazers zile koti ndogo tulizozoea. Hivi vitu ni magic, hutransform outfit kwa namna ya kipekee.Ukiwa na boyfriend jeans ukavaa tshirt na ndala utaonekana wa kawaida ila the moment unavaa pointy shoes kama stilleto afu ukatupia koti flan amazing na bold lipstick basi unatoka kwenye 2/10 to 10/10. Tena hivi vitu hufanya uonekane like u look good without a lot of effort. Effortless elegance.
A touch of trendy items ambazo hazijawa overused na watu
Jaribu kununua some trendy outfits au trendy accessories. Kuna mikanda, handbags, shades na hereni nzuri sana ambazo zimetrend lakini hazijavaliwa kupita kiasi. Please hapa siongelei fake fenty au zile fake gucci waist bags wala offwhite belts but naongelea like bamboo earings, kuna bags flan kama za mkeka, yani zaidi invest kwenye trends zenye options nyingi ili hata ukivaa isiwe kitukile kile yule nanii kavaa.
Achana na dar oye
Kuna zile nguo mara nyingi huuzwa kariakoo, yani ikitoka kila mtu anavaa na ukitembea unakutana na watu kadhaa wamevaa. Achana na hizi nguo, yani nguo ukitembea kila mtu anaijua hadi bei. Nguo ikivalika sana inapoteza hata uzuri wake na thamani. Watu ghari hawavai vitu ambavyo kila mtu anavyo. Imagine unatembea zako uependeza na kishati chako afu unakutana na watoto wameuramba na shati hilo hilo, story of my life. Sasa that feeling sio nzuri na you feel cheap.
Mtumie fundi cherehani, fit ni muhimu
Nguo inayokutosha vizuri huongeza thamani, peleka basi hizo suruali zinazokulegea kwa fundi. Na hiyo gauni ina mikono mikubwa ifanyie utaratibu ifiti kila kona ya mwili wako vizuri. Nguo zinazobana sana au kupwaya wakati sio mtindo wake hufanya mtu aonekane rough na asojali. Unaponunua nguo ka haitoshi usiache kupeleka kwa fundi kabla ya kuvaa
Usiover match wala kuover accessorize
Less is more. Kuna vitu ukifanya tu mtu anaona umepania au hujui unalofanya. Usilamizishe kuvaa accessories zote ulizonazo kwenye vazi moja na kuvaa rangi zinazofanana sana, yani shati nyekundu, kiatu na mkoba vyekundu, hereni nyekundu, rangi ya kucha nyekundu. Huu ni ushamba. Try to combine colours na pia vitambaa mbalimbali vya nguo sio kila kitu cotton from head to toe. Pia jua uvae accessory ipi kwenye nini, nimeona watu wakivaa official wear na cultures ambazo zinastail kuvalika kwenye casual wear au classy dress na shangshanga zisizoeleweka
Makeup na manukato
How you smell tells a lot kukuhusu. Nunua perfume yako au body spray yenye harufu nzuri iliyotulia, sio uvunje kibubu kisa perfume ila pia usinunue very cheap au yenye harufu cheap. Ushawahi sikia mtu ana harufu flani ukajua tu katoka gesti ya kitaani au harufu kama za babycare. Kuna baadhi tu ya harufu zinascream cheap. So nunua kitu cha bei ndogo lakini harufu yake iwe imetulia. Hii itasaidia kucompliment muonekano wako wote. Mara nyingi mtu akikuangslia uwa kichwani inajijenga imani juu ya harufu yako. Sasa ukivaa fresh afu harufu ikapingana na wewe basi inakua sio poa. Please usipake makeup kama unaenda kwenye harusi, more is not better. Paka makeup inayoendana na tukio. Kuna nguo unaweza iharibu kwa kupaka too much or very little makeup
Jari nywele zako
Nywele ni muhimu na nywele huongea mengi sana kukuhusu. Hata upendeze vipi nywele zinaweza haribu the whole look. Cheap huonekana tu. Usidhani watu hawaoni hizo nyuzi za weaving ulixoamua kuziacha juu au labda hatujaona gundi inayobanduka kwenye wig lako. Chana nywele, zimefumuka repair. Acha kuweka style na rangi za ajabu. Na kaa mbali na rangi nyingi nyingi kichwani wewe sio salad hata. Kijani unataka, nyekundu, njano zote kwenye kichwa kimoja. Pia hakikisha unaweka rangi inayoendana na ngozi yako sio unalazimisha blonde hair wakati haicompliment ngozi yako. Hakikisha nywele zako ziko neat, sio lazima uweke lace wig.
Nunua mtumba grade A
Lengo kubwa ni kupendeza bila kugharamika, nguo za mtumba zenye ubora zitakunufaisha sana. Kwanza kuna mitindo mingi kwenye mtumba na ni vigumu kukutana na mtu aliyevaa nguo kama yako. Kuna
designer wear kwenye mtumba, yali yale mavazi yaliyobuniwa na watu wakubwa tofauti ni lwamba tu kuna mtu alikusaidia kuvaa kigodo. Kuna nguo nyingi za mtumba ambazo huvutia kuliko za dukani na cha muhimu ni utapendeza kwa bei chee. So usisite kununua.
Related posts
1 Comment
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/look-expensive-for-less/ […]