SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Looks From BSS 2023 Launch
Mitindo

Looks From BSS 2023 Launch 

Msimu mpya wa Bongo Star Search umeanza na mwaka huu kuna ma judge watatu ambao ni Rita Paulsen, Salama Jabir na Shilole wakati host wa show akijirudia tena Meena Ally.

Katika kuzindua msimu huu mpya kulikuwa na launch day lakini pia kulikuwa na poster ambayo ilitembea mtandaoni ikionyesha judges na host wa msimu huu mpya, kwenye yote haya tumeona mavazi yao na tukaona sio mbaya tu-review

Tukianza na poster, inaonyesha mwaka huu wametaka kuwa ki-Africa zaidi na inatuma vibe ya miaka 80, colorful outfits, tumeona kitenge lakini pia tumemuona shishi na gele kichwani.

Rita Paulsen alikuwa amevalia cold shoulder mixed prints kitenge dress, akiwa ame match gauni yake hio na kilemba kichwani, amemalizia muonekano wake na mkufu na catch makeup, amependeza sana,

Salama yeye alivalia colorful suit, amevaa coat ya kijani, top nyeupe suruali ya blue amemalizia muonekano wake na black & white shoes huku akiwa na beaded layared necklaces, ankara pocket square na red gloves, tunadhani angetoa hizi gloves na hizo cheni angependeza zaidi, angekuwa clean.

Master Jay yeye nae alikuwa kwenye colorful fit, check trouser, purple coat, white shirt amemalizia muonekano wake na vans zenye weusi,njano na nyeupe, socks nyeusi na ankara pocket square pamoja na glasses.

Shilole alivalia full yellow fit hakuwa na mambo mengi na amependeza.

Meena amevalia front slit dress ambayo ime mixiwa na kitenge, showing cleavage, amevaa vazi hili na kilemba, hereni zilizo match na gauni akamalizia na bangili pamoja na black open sandals.

Wakati siku ya launch mionekano yao ilikuwa hivi,

Master Jay looked sharp in a blue suit, viatu vyeusi akamaliza na black shoes, Salama alikuwa in full black look black suit, black shoes, black cross body bag na amemalizia muonekano wake na miwani, Meena alivalia gauni yapink amemaliza muonekano wake na open heels za orange,Rita alivalia purple suit, green pumps amemaliza muonekano wake na top nyeupe, saa, bob hair cut na simple makeup.

Shilole alivalia denim on denim look tunaweza kusema haku-get the memo maana wengine wote wamevalia formal yeye yupo casual, japo alipendeza na vazi lake lakini ameharibu look ya theme nzima.

Anyways tuambie umependa look za nani katika picha zote mbili?

Related posts