SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MAKEKE NA MAKEKE YAKE KATIKA UBUNIFU
Ana Kwa Ana

MAKEKE NA MAKEKE YAKE KATIKA UBUNIFU 

AfroSwagga katika Ana Kwa Ana imefanya mahojiano kwanjia ya mtandao na Msanii wa mitindo kama ambavyo napenda kuitwa yeye mwenye Bwa. Jocktan Maluli, maarufu kama MAKEKE, Pata kujua kafunguka yapi mbunifu huyu mwenye hasira na kazi yake.

 

10422151_402851556550884_7840960835066996402_n

 

AfroSwagga: Makeke ni nani?

Makeke: Makeke ni msanii wa mitindo ambaye anafanya  mitindo ya kiafrika/kiasili kutokana na maisha ya Muafrika halisi, Jina kamili ni Jocktan Cosmas Maluli amabaye pia ni mmiliki wa kampuni ya MAKEKE AFRIKA CO.LTD iliyopo Boko  – Dar es salaam ambayo ilianzishwa mapema mwaka 2012 December, mpaka sasa inakaribia kuwa na miaka 3, Kampuni hii ina idara tatu muhimu amabazo ni MAKEKE AFRIKA KOLEKSHENI, MAKEKE MEDIA & MAKEKEMODELING AGENCY.

 

AfroSwagga: Ubunifu umehifunzia wapi?

Makeke: Jocktan Maluli/ Makeke alikuwa na kipaji cha uchoraji tangu akiwa mdogo, na alishawahi kuwa mchoraji bora wa shule ya msingi wakati huo akiwa Mbeya, Pia kidato cha nne na kidato cha sita alipoibuka kuwa mchoraji bora wa katuni nyanda za juu kusini na Tanzania kwa ujumla na kuzawadiwa pesa na cheti na taasisi ya kuzuia rushwa takukuru, wakati huo akiwa kidato cha tano na cha sita ndipo alipoanza kufanya mitindo kama MODEL na akafanikiwa kuwa Mr. Mbalizi high school wakati huo na Mr.Mbeya vijijini hapo ndipo alipopewa jina la model makeke kutokana na miondoko yake jukwaani, baadae alianza kushauriwa na watu kuwa kutokana na uwezo mkubwa wa kuchora anaweza kuwa mbunifu mzuri wa mavazi basi toka hapo ndo akaanza rasmi ubunifu wa na watu walikuwa wakikubali kazi zake, baadae akafanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha Dododma (UDOM) ambapo alikuwa akisomea Shahada ya (FINE ARTS & DESIGN) na hapo ndipo haswa alipotimiza ndoto zake za kuwa msanii bora wa mitindo, baadae akajiunga na AFRIKA SANA chini ya mbunifu ALILNDA SAWE kwa ajili ya mazoezi ya vitendo.

11010603_450235418479164_8449276858023132973_n

 

AfroSwagga: Umejikita katika nyanja moja au zote za ubunifu?

Makeke: Aina mbali mbali, ubunifu wa nguo, ubunifu wa mapambo ya ndani pamoja na kupamba kuta, graphics design, make up design

 

AfroSwagga: Kwanini nyanja zote?

Makeke: Zote, kwasababu toka nikiwa mdogo nilikuwa katika mazingira hayo ya kujifunza vitu vingi, na pia chuo kikuu tulikuwa tukisoma aina mbali mbali za sanaa.

unnamed

 

AfroSwagga: Umewahi kushiriki katika majukwaa mengi ya mitindo ndani na nje ya nchi. lakini cha kushangaza MAKEKE bado ni jina geni kwa Watanzania walio wengi. Hii inasababishwa na nini unadhani?

Makeke: Kikubwa nafikiri watu bado hawajaelewa vile mimi nafanya mambo yangu, na pia hawajaelewa hichi kitu nnachokiita sanaa ya nguo, kiukweli sipendi kuitwa designer napenda mtu aniite artist, kwahio am a fashion artist nafanya kitu kwa uwezo zaidi ya ule wa designer, coz designers wengi wamekuwa watu wa ku copy na ku pest (bandika bandua) yaani hawaumizi kichwa katika kufanya michoro yao, mimi sina mipaka katika kufanya nguo naweza tengeneza nguo katika mazingira yoyote kwa material yeyote, Pia watu bado hawajanielewa kwasababu nafanya mitindo migumu ingekuwa ni muziki basi ni muziki wa TAMADUNI MUSIC nguo nyingi si rahisi kuvalika mtaani.

– industry ya mitindo Tanzania iko katika matabaka , wanamitindo wengi wanajiona kama miungu kitu ambacho sikipendi  na ndio maana niko mbali na watu wa tabia hiyo na hii ndo sababu ya kwenda kufanyia mitindo nje kwani watu wako makini na wanakuelewa kuliko nyumbani.

– Media zinabana sana

– Pia sina muda mrefu kwenye industry

– pia nilikuwa sijajua kutumia njia nzuri za kujitangaza

mail.google.com2

 

AfroSwagga: Ukitoa ubunifu shughuli gani nyine unafanya?

Makeke: Nje ya ubunifu nafanya

– painting

– illustration & cartoon

– photography

– graphics design

*ukichek hivyo vyote vinazama kwenye sanaa , na hii ndo maana ya kuitwa msanii

 

AfroSwagga: Tofauti yako wewe na wabunifu wengine?

Makeke: Tofauti kubwa ni kitu kimoja nakiita CREATIVE& ARTISTIC MINDS, nna uwezo wa kubuni na pia nna chembe chembe za kisanii ndani yangu ndio maana hata kazi zetu hazifanani

– tofauti ya pili ni kwamba wao wanafanya mitindo kama kazi ya ziada lakini kwangu ni kazi ya kwanza , IAM A PROFFESSIONAL.

– Tofaut nyingine ni kwamba wanafanya kwa ajili ya wakati huu mm nafanya kwa future so niko naona mbali.

mail.google.com7

 

AfroSwagga: Tovuti uliyoweka katika ukurasa wako wa Instagram haifunguki, na siku hizi biashara imehamia zaidi katika mtandao umejipanga vipi kwa ilo, Je, unampango wowote wa kufungua tovuti itakayokuwa inakutangaza wewe na bidhaa zako?

Makeke: Yaah ni kweli tovuti ile haifunguki na hii imetokana na matatizo ya kiufundi kwa yule mtaalamu aliyekuwa akiitengeneza lakini itatengamaa muda si mrefu.

 

AfroSwagga: Mara ya mwisho kushiriki katika jukwaa la mitindo ilikuwa lini? na nini kinafata kutoka kwako?

Makeke: Mara ya mwisho ilikuwa tarehe 4/7/2015 NAIROBI  – SLUM FASHION AFRICA – KENYA. na kwa sasa kuna show nyingine nyingi zinafuata kama , KISUMU FASHION WEEK – september 5, FASHION& STYLE EXPO –      NAIROBI, THE DESIGNER WALK FASHION SHOW – TDWFS – South Africa, ABUJA INTERNATIONAL FASHION WEEK – NIGERIA,  EAST AFRICA MOTOR SHOW – NAIROBI, pia kutakuwa na uzinduzi wa brand yangu mpya ya BUTTERFLY BRAND – December,

IMG-20150706-WA0019-750x500

 

AfroSwagga: Je, wewe ni mmoja wapo kati ya wabunifu wanaobuni mavazi ya kulingana na misimu ya hali ya hewa?

Makeke: Hapana mimi nabuni kutokana na maisha ya ya muafrika , Hasira, na ndoto        zangu mwenyewe bila kujali ni msimu gani wa hali ya hewa.

makeke-designs

 

AfroSwagga: Tunaona wabunifu wengi katika kujitangaza wao na kazi zao, wanatumia sana lebo ambazo wanazibandika katika mavazi na bidhaa zao, Je, wewe unatumia mbinu hii katika bidhaa zako?

Makeke: Kipindi cha nyuma sijatumia ila kwa saa nimeanza kutumia kwenye mzigo wangu mpya wa BUTTERFLY                      BRAND.

mail.google.com

kazi nyingine za makeke

mail.google.com1

 

mail.google.com5

mail.google.com15

Bila shaka umefurahia mahojiano hayo mafupi ambayo yatapata kukupa mwanga kama ulikuwa umfahamu basi tayari ushalijua jina la MAKEKE na siku nyingine hautastuka utakapolisikia na kama ulikuwa tayari unamfahamu basi umeongezea katika kile ulichonacho. Rai yangu kwa watanzania wote ni Kuthamini kilicho chetu kwanza, alafu vingine vifuate. Asante! UNAWEZA KUMFOLLOW FACEBOOK Jocktan

Wa  Makeke  Afrika, ISTAGRAM @iam_makeke_from_tanzania

Related posts

6 Comments

  1. here

    … [Trackback]

    […] Here you can find 99848 additional Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/makeke-na-makeke-yake-katika-ubunifu/ […]

  2. original willy wonka

    … [Trackback]

    […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/makeke-na-makeke-yake-katika-ubunifu/ […]

  3. magic mushrooms blue meanies

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/makeke-na-makeke-yake-katika-ubunifu/ […]

  4. Continue Reading

    … [Trackback]

    […] Here you will find 58483 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/makeke-na-makeke-yake-katika-ubunifu/ […]

  5. 토렌트 다운

    … [Trackback]

    […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/makeke-na-makeke-yake-katika-ubunifu/ […]

  6. Medicijnen bestellen zonder recept bij Benu apotheek vervanger gevestigd in Amersfoort

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/makeke-na-makeke-yake-katika-ubunifu/ […]

Leave a Reply