SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Makosa Ya Style Yanayo Fanya Uonekane Cheap
Mitindo

Makosa Ya Style Yanayo Fanya Uonekane Cheap 

Ninapenda hizi nyakati tunazoishi, I really do. You can be anything…anything you chose to be. Isn’t it just lovely. Unaweza kuwa a strong independent woman, a funky chic, boho with a touch of sexy, unaweza kuwa chochote ikiwemo kuwa cheap, miserable, low value, careless n,k. Kwasababu ya uhuru huu hii article ni kwa ajili ya wanawake wasiopenda kuonekana cheap. Wanawake wanaopenda kuwa classy and elegant au kujifunza kuwa hivi. I respect maamuzi ya mtu but kumbuka kuwa maamuzi yana impact..kila unachochagua kina mchango katika kujenga au kubomoa so chose wisely baby. So kwako wewe classy, elegant babe tuendelee. We dress everyday, kwa ajili ya matukio mbalimbali. Mavazi ni utambulisho, kwa sababu mbalimbali ni vyema kutambulishwa katika namna ambayo ni sahihi. We are not perfect, baadhi ya makosa ya kimitindo tunayoyafanya huwa yanafanya tuonekane cheap au tunaseek sana attention(dalili ya vitu cheap)

Kuvaa Fake Brand Clothes ( Full)

Hakuna kitu kinascream cheap kama logo  kubwa za  luxurious brand kwenye  nguo fake. Let me make it clear..I wear fakes na dupes pia coz your gal ain’t a millionaire..YET, na kuna designs nazipenda sana ila ndio original siwezi kuafford kwa sasa so a girl  gotta do what a girl gotta do hahaa. Ila haya mambo ya kuvaa logo juu mpaka chini au logo kubwa kweli mpaka attention yote ipo kwenye brand name sio kabisa. Mtu akikutazama unaonekana ulivyo proud na hizo nembo mwilini like unafanya juu chini tuzione kwa zilivyo nyingi au zilivyo kubwa.

Girl who you trying to lie to. Au kuvaa logo za brand tofauti tofauti at the same time. Top ya DnG, Suruali Gucci, Sandals LV..yani hata kama ni original usivae hivi , ni kupania huku. Na kupania looks cheap, kuvaa logo nyingi tena feki ndio cheap kwelikweli. Kama unavaa fake yenye logo kubwa ( na isiwe kubwa kupitiliza) angalau vaa moja na kama ni ndogo sana angalau mbili. If possible kaa mbali na fakes zenye logo zinazoonekana. Ukitaka kujua kuvaa better make sure you follow us on instagram at elegancebyree.

 • Kuvaa Nguo Zinazoonyesha Maumbile Yasiyo Sahihi Kwa Kiasi Kikubwa

We all want to look sexy and attractive. Kila mwanamke anapenda kuwa na mvuto but listen boo, KUWA SEXY SIO LAZIMA UONESHE MAUMBILE YAKO YOTE. Classy women wanavaa sexy, kina Faranja Nyarandu, Jackline Mengi and the like. Siku zote they look elegant na mara nyingi tu they look sexy. Angalia wake wa maraisi wa nje, important stylish figures. Wengi sana wanavaa sexy na wako attractive but kiukweli hutoona any of them wakiwa wameachia viungo vyao vyote nje. Kuonesha maumbile sana inaonesha uko desperate and you are thirsty na Classy women hawana kiu ya unnecessary au wrong attention.

So kuna siri katika kuwa sexy but classy, Unapovaa chagua sehemu moja tu ya kuonesha, sehemu ya kuringishia watu. So inaweza kuwa the curves au waswahili tunaita nyonga ukavaa tight dress, au the legs ukavaa nguo fupi ila ikacover  juu, au cleavage ukava kifua wazi kidogo huku umeboost na ukavaa nguo isiyoacha miguu wazi sana. Pia ukivaa nguo fupi jitahidi isibane sana. Kama nilivyoandika, usioneshe maumbile sana sehemu zisizo sahihi so kuna exception, yani sehemu kama club na beach n.k

 • Too Much Anything Hasahasa Makeup & Accessories

Kuna kitu kinaitwa poor people mentality. Ushawahi kukutana na memes zinaonesha mtu asiye na hela kavaa simple ila maskinii ana bling bling za hatari? Basi mentality hiyo ni kuwa maskini wengi wanaamini kuwa ili waonekane wanavyo ni lazima waonyeshe lakini wenye nazo hawajaribu kudhihirisha but wanajua tu wanazo. Classy women wana rich peoples mindset, hata katika uvaaji na hata kama they are not making millions kwa sasa (they will eventually).

So classy women hawajaribu kuweka too much of anything hususani sehemu zisizo stahili. Hakuna haja ya kuweka makeup nyingi sana kwenda kazini tu, umecontour na kuhighlight na eyeshadow za marangi. Hakuna haja ya kope ndefu sana hadi mtu akuone umeweka hata kwa mbali, no need ya contact lens yenye rangi kali sana. Hakuna ulazima wa kuvaa cheni, herein, bangili, saa vyote kwa pamoja. Too much of anything haiwezi kupendeza na mwisho wa siku unaonekana kama you are trying too hard wakati classy outfits look effortless. I want to see you dress classy, yani upendeze na uvutie pia ndio maana nashare tips mbalimbali juu ya uvaaji kupitia instagram at elegancebyree

 • Kulazimisha Kitu Sehemu Isiyosahihi

Heheheee, kuna vitu unajikuta umenunua lakini hujui hata utavalia wapi au utavaa na nini. Ukikiangalia kivazi kinavutia kwelikweli na unatamani sana kukivaa lakini pa kukivaa na kukivalia ni kesi. Maybe ni top Fulani imekaa kiclub sana na  lets say ina maneno yasiyofaa. Siku Fulani unajitosa unakipigilia alafu unaassume watu hawaelewi kizungu au watapotezea, club macho kwako. Kaka wa watu anaamua kukuuliza, dada are you a stripper kweli au ni nguo tu inasema hivyo. Case kama hizi ziko nyingi, unalazimisha kuvaa blazer au koti na sandals. Unaforce nywele haziendani au accessories haziendani na nguo na huwezi kuvaa hiyo evening dress bila nakshi so unajiambia to hell unavaa. Watu wananotice asikwambie mtu, wewe unaweza kukausha but hata wanaume huona baadhi ya viu vikiwa forced. Swali linabak huyu dada hana nguo, hana nakshi, haelewi anachofanya au?

I hope umejifunza kitu kutoka katika hili, I want you look better, feel better and do better babe. I hope unataka the same kwa ajili ya wanawake walioko maishani mwako. If you do please share the article and follow me at elegancebyree instagram. Unaweza kushare link on whatsapp, email, insta e.t.c

Related posts

3 Comments

 1. buy benelli shotguns

  … [Trackback]

  […] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/makosa-ya-style-yanayo-fanya-uonekane-cheap/ […]

 2. 티비위키

  … [Trackback]

  […] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/makosa-ya-style-yanayo-fanya-uonekane-cheap/ […]

 3. Mushroom liberty cap

  … [Trackback]

  […] Here you can find 24295 additional Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/makosa-ya-style-yanayo-fanya-uonekane-cheap/ […]

Comments are closed.