Wa-Africa wengi huwa hatuna utaratibu wa kujiweka madhumuni na hii sio tu katika kufikia malengo ya biashara au elimu bali hata katika mavazi yetu binafsi, wengi tunafanya kitu kikitokea tunahitaji kukifanya mfano: hatujiwekei malengo ya unafanya shopping mara ngapi kwa mwaka na katika shopping hio unataka kununua kipi na kipi ili kufikia lengo la muonekano upi?
Umasikini au kutokuwa na pesa ni sababu kubwa ya watu kusema sipendezi sababu mimi masikini, lol we don’t mean to laugh lakini kama ukijiwekea malengo ukaamua kuyafata serious basi inawezekana usiwe hata na shilingi kumi mfukoni lakini watu wakakuona kama una millioni mfukoni mwako as mababu zetu walisema “umaridadi uficha umasikini”, Well acha tukupe malengo kumi unaweza kujiwekea mwakani ukaanza mwaka wako na kuumaliza maridadi kabisa.
- Angalia nini kinafaa na nini hakifai
Kwa kuanza ni vyema ukaanza na kuangalia kabati lako la sasa, kipi kinafaa kuvuka kwenda mwaka 2019 na kipi kibaki, hii itakupa nafasi ya kuingiza vipya na kuondoa vile ambavyo havina maana. Lakini pia kukupa nafasi ya nini kinahitajika kimepungua na kipi kinatosha,unaweza kuendelea na utaratibu huu hata baada ya mwaka mpya jaribu kusafisha kabati lako kila mwezi ili kuondoa ambavyo havina maana.
- Fanya manunuzi kwa ungalifu
Sio kila kitu lazima ununue hata kama hakiitajiki, ni bora kuwa na vichache vyenye muonekano mzuri kuliko vingi vilivyo choka, nunua vitu bora ( quality over quantity) ambavyo vinaweza kukaa miezi mingi ili kuepusha shopping za mara kwa mara zisizo na kichwa wala miguu, wakati wa manunuzi angalia hicho ununuacho kinaweza kuvaliwa zaidi ya mara mbili katika occasion tofauti? mfano: Shirt nyeupe inaweza kuvaliwa kazini, casual na hata katika mikutano na familia, a black pump pia unaweza kuivaa na kuitumia mara nyingi uwezavyo,Invest in quality na zinazowezekana kuvalika mara nyingi.
- Fikiri Unataka Kuwa Na Muonekano Upi
We all have different taste’s linapokuja katika swala la style and fashion, jaribu kufikiri wewe upo comfortable na style gani? hapa ndipo wengi tunapo pashindwa utakuta tunapelekeshwa na trend unajikuta una mavazi mengi lakini yote si style yako unaishia kuyaweka kabatini au kugawa (waste of money) badala ya kufanya hivyo fikiri unataka ku-achieve muonekano gani 2019 ambao utaongea kuhusu wewe, je are you more of a casual person? Chic? Fancy? chochote ambacho kitakutambulisha basi chagua hiko na hakikisha ukienda kwenye manunuzi unachagua mavazi ambayo yanaendana na style yako.
- Color Choices & Body Type Ni Muhimu
Kujua una type ipi ya mwili na rangi ukizipendazo ni muhimu pia, hii itasaidia pale katika ku-shop smart, unanunua mavazi ambayo yanaendana na wewe na utayavaa kila mara, well kuna watu ambao hawana mapenzi na rangi fulani basi si vyema kuji-force kuivaa sababu tu labda ipo kwenye trend, unanunua vazi ambalo haliendani na mwili wako linaishia kwenye kabati ni utumiaji mbaya wa pesa na kujijazia vitu visivyo tumika, buy what you can wear a million times.
Jua Aina Ya Mwili Wako Na Mavazi Yanayo Kufaa
- Accessorize More
Wa-Africa wengi tuna kimbia swala la ku-accessorize na hapa hatumaanishi tu cheni na hereni, kuna vitu vidogo vidogo ambavyo vinaweza kubeba muonekano wako kama, mkanda, pochi, blazer, scarf, saa, vibanio vya nywele,miwani na vingine vingi. Utakuta mtu amevaa tu suruali yake, shirt na viatu anatoka yes unaweza kuwa umependeza lakini kumbe ungeongeza na saa, mkanda na koti basi unge stand out. Mwaka huu jaribu kuongezea vitu tofauti tofauti katika muonekano wako, spice it up.
- Take Risk
Wengi huwa tunaji-limit unaweza kukuta umependa sana vazi fulani lakini utasikia “bongo hii ntalivaa wapi”? kwanini usiseme acha niwaonyeshe namna ambavyo unaweza kuvaa hili vazi hapahapa bongo na ukaeleweka? sometimes tunafikiri sana kuhusu watu kuliko kujifikiria sisi wenyewe kila mtu ana uhuru wake, you’re i can’t is someone else can, take risk and show them how its done.
- Stop Following Fashion Rules
For one to stand out he/she must break the rules in a good way, some choose to be in the comfort zone few are stepping out of them, hao wachache ndio ambao leo tunawaita fashion icon’s kwa maana wao wapo tofauti na wengine. Hapa hatumaanishi uvae vitu visivyo eleweka hapana lakini kama unaweza kuvaa shirt mbele kukawa nyuma na nyuma kukawa mbele na ukapendeza then why not? nani amesema fashion ni mathematics jamani kwamba lazima jibu lifanane? what you need is to do it & look good basi.
- Ditch The Trend
Unless ni trend ambayo inaendana na wewe na unaweza kuivaa tofauti then unaweza kuifuata lakini kama ni trend ambayo haina muingiliano na muonekano wako save them coins for something better, unachotakiwa kukumbuka ni kwamba trend’s come and go na chache ni zile ambazo hata zikiondoka unaweza kuvaa tena bila kuwa judged nyingi zikienda zimeenda.
- Shoes Shoes Shoes
Invest kwenye viatu, viatu ni muhimu sana katika muonekano wako, they can upgrade and down grade a outfit, make sure unanunua vile ambavyo upo comfortable navyo.
- Make A Statement & Try New Things
Katika outfit yako hakikisha una weka statement katika kila outfit yako, mfano kwenye outfit ambayo ina rangi zilizo fade unaweza kuongezea kiatu chenye rangi ya kung’aa na kuwa statement ya outfit yako, unaweza kubeba pochi ambayo ina make statement, belt etc. Make sure unakimoja ambacho kitabeba wengine.
NOTE: Comfort is everything, kwenye kila hatua unayofanya katika ku-upgrade kabati lako na style yako mwakani upo comfortable nacho.
Related posts
4 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/mitindo/malengo-kumi-10-ya-kujiwekea-kwa-ajili-ya-kuanza-mwaka-mpya-kwa-umaridadi/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/mitindo/malengo-kumi-10-ya-kujiwekea-kwa-ajili-ya-kuanza-mwaka-mpya-kwa-umaridadi/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/mitindo/malengo-kumi-10-ya-kujiwekea-kwa-ajili-ya-kuanza-mwaka-mpya-kwa-umaridadi/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/mitindo/malengo-kumi-10-ya-kujiwekea-kwa-ajili-ya-kuanza-mwaka-mpya-kwa-umaridadi/ […]