SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Maoni yetu kwa washiriki wa Miss Tanzania 2018
Mitindo

Maoni yetu kwa washiriki wa Miss Tanzania 2018 

Haya ni maoni yetu kwa washiriki wote wa Miss Tanzania 2018. Kwanza kabisa tunatoa kudos kwa kila fashion blogs, beauty pageants page’s, na kila ambae anachukua muda wake kujaribu kutoa ideas zake kuhusu miss Tanzania. Tumekuwa tukiisubiri kwa hamu toka Lundenga ajiuzuru na hii ni kutokana na kwamba wengi tunaipenda na tungependa kuona mabadiliko. Uchaguzi wa mikoa umeisha na sasa tunaingia kufanya uchaguzi wa kanda kabla hatujaingia katika mtanange wenyewe wa miss Tanzania.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo sisi kama Afroswagga tungependa kuona yanabadilika;

  • Nywele na makeup  

Kama miss Tanzania huwa ina mtu au huwa ma-miss wanachukua watu wao binafsi please make sure unachukua mtu ambae anauelewa na hivi vitu darlings tumechoka kuona style’s za nywele za send off kwa ma miss hivi ni kwanini hatujifunzi kwa kuangalia wenzetu? utakuta ma-miss wote wana style za nywele aina moja tena ya send-off, tumechoka give us something new,pia uchaguzi wa rangi za hizi nywele na quality girls please kuna nywele za kila aina za quality nzuri please hizo mbagala oye ziacheni kwanza. Kwenye makeup ziendane na rangi za ngozi za washiriki zionyeshe uzuri wao sio kumb’adilisha au kumpaka makeup nyingi mpaka anaonekana age go.

  • Mavazi Ya Ubunifu & Evening Dress 

Ukiambiwa vazi la ubunifu ni kwamba tunataka ubunifu, kitu kipya haya mavazi ya viroba, majani ya mgomba, magazeti  yamesha pitwa na wakati au kama ungependa kufanya hivi basi give us something to talk about, we need creativity inawezekana ukashona vazi lako la kitambaa ila likawa na creativity kuliko hio migomba na viroba, wabunifu wengi wapo ambao wanauwezo wa kukupa kitu cha tofauti kama Makeke International etc.

  • Evening Dress 

Hapa wengi wanajitaidi kitu ambacho tuna tatizo nacho ni kushikilia ile nguo wengi huwa wanapenda kuzishikilia ili wapate kutembea vizuri, girl chagua kitu ambacho kitakufanya uwe comfortable katika kutembea ukiachana na urembo wako na akili tunaangalia pia the way you own the stage sasa unaawezaje ku-own stage kwa kushikiria gauni? na ukishalinunua fanya mazoezi ya kutembea nalo hata nyumbani kwenu hii inakua urahisi siku ambayo utapanda nalo jukwaani unakuwa umeshajua flaws zake.  Inawezekana ni lazima yawe marefu lakini kama fupi lina ruhusiwa rock it & be different

  • Viatu

Hapa jamani hapa muangalie sana please nunueni viatu mnavyoweza kutembelea, kiukweli kama wewe ni mfupi kidogo utaendelea kuwa hivyo usitake kuvaa magongo kuwadanganya ma judge by the way watakuwa wanajua kimo chako kabla ya kupanda jukwaani,

kuna hii design ya viatu tumekuwa tukiiona mnaipenda kweli ni ndefu lakini sio flattering havina mvuto kabisa,pia muangalie muingiliano wa mavazi yenu na viatu we swear hili ni tatizo kubwa sana, mtu kavaa kijani viatu njano kisa tu kavaa gauni refu anajua havito onekana

 

 

Related posts