SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Martin Kadinda ” Kwa Sasa Tanzania Hakuna Tofauti Ya Wabunifu Na Mafundi Cherehani”
Habari

Martin Kadinda ” Kwa Sasa Tanzania Hakuna Tofauti Ya Wabunifu Na Mafundi Cherehani” 

Marin Kadinda ni moja kati ya wabunifu wakubwa kabisa Tanzania, Kajipatia jina kubwa kupitia kazi yake ya ubunifu lakini je hili swala la wa Tanzania kulalamikia kazi zao na kusema “hamna wabunifu kuna mafundi cherehani” na kwamba “wabunifu Tanzania wana igiziana kazi zao” yeye ana liongeleaje?

Afroswagga: Martin kama mbunifu ambae ume tumia nguvu na kipaji chako cha ubunifu kufika hapa ulipo leo halafu una sikia kwamba wa Tanzania wanasema siku hizi hakuna wabunifu kuna mafundi cherehani una onaje au kuliongeleaje hili?

Martin Kwasasa tanzania hakuna wabunifu kuna mafundi cherehani..? Kwanza kabisa ubunifu ni uwanja mkubwa sana ambapo kwa macho ya kawaida huwezi kuona.. fundi kuweka kushona mitindo mbali mbali hakumfanyi kuwa mbunifu.. uwezo kwa kubuni mchanganyiko mpya wa vitambaa.. vifungo.. zipu na malighafi mengine katika kazi ya ushonaji ndo kunakufanya kuwa na uelewa wa ubunifu.. ila pale unapochukua ufundi kushona, ubunifu wa vitu nilivyovitaja hapo na kuvifanya mtaji wa biashara

Ndo vinakufanya kusimama kama mbunifu wa mavazi… kipaji chako kinageuka kuwa ajira

Kwa kuzingatia hilo mafundi wengi wanalewa sifa kwakuwa wanauwezo wa kunakili kazi za wabunifu na wao wanajiona ni wabunifu.. sidhani kama ni kosa au  wanapaswa kubezwa.. ningependekeza wawekezaji wakaona fursa kwa mafundi hawa kukusanywa na kuwezeshwa hata kwa viwanda vidogo kuweza kuboresha kazi na kuziuza kwa bei nzuri ili industry yetu ikue..

Sitegemei kama ni vyema kudiscuss about hakuna wabunifu, kuna mafundi cherehani kama ni suluhisho ila maswali yetu yawe wanafocus upande wa pili wa shilingi kuweza kuwasaidia hawa mafundi chelehani zaidi kukua

Afroswagga: Je vipi kuhusu kuigiana kazi?

2. Wabunifu kuigana kazi..? Sidhani kama ni kuigana ila naona ni mawazo au fikra kuendana tu.. unapoitwa mbunifu tayari inaonesha una karama ndani yako ya kubuni ila pale mawazo yanapogongana na mawazo ya mbunifu mwingine hicho ni kitu kizuri maana uwezo wa kuboresha kilichobuniwa na malighafi zilizotumika ndo kunanogesha kazi

Najua kuigana kupo ila sidhani kama kunaathiri ila sana sana kunakufanya mbunifu kubuni vitu vigumu zaidi kuliko mwanzo ili usiibiwe ubunifu wako

Martin asante kwa muda wako tuna appreciate kwa kuchukua muda wako kutufumbua macho kuhusu swala hili. Ps: tuna subiri new collection

Related posts

1 Comment

  1. Full Report

    … [Trackback]

    […] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/mitindo/martin-kadinda-kwa-sasa-tanzania-hakuna-tofauti-ya-wabunifu-na-mafundi-cherehani/ […]

Leave a Reply