SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Maswali Ya Kujiuliza Kabla Hujanunua Kitu Kinacho Trend
Mitindo

Maswali Ya Kujiuliza Kabla Hujanunua Kitu Kinacho Trend 

Kuna msemo unasema miluzi mingi ina mpoteza mbwa, yes hii ni kweli kabisa na sio tu katika maisha bali katika mitindo na urembo pia.

Unaweza kukuta aina fulani ya vazi au urembo unakuwa hyped na fashionista’s, Influencers etc na wewe ukaona ununue uvae.

Sio mbaya ku keep up na fashion lakini kabla ya kufanya maamuzi ya kununua kitu hiko Jiulize maswali haya manne


1) Je Inasupport Aina Ya Mwili Wako?

Sote tuna support body positivity lakini kuna vitu mtu wa mwili wa aina fulani akivaa anaweza kushangaza wengine, sio kila kitu kinaweza kuvaliwa na kila mtu.
Unaweza kununua hiko kitu kwa bei ghali na usikivae sababu ukaona hupendezi
Ukakivaa lakini usiwe comfortable nacho hakikisha trend inayoendelea inafaa mwili wako.


DondooJua Aina Ya Mwili Wako Na Mavazi Yanayo Kufaa

2) Je ina compliment style yako?

Hii pia ni muhimu mfano wewe ni mtu wa viatu vifupi unaona trend ya highheels kila mtu anavaa basi na wewe unakimbilia kununua matokeo yake viatu vinaishia kuchubuka kwenye shoe rack huvivai. Hakikisha kabla hujarukia trend iwe ina compliment style yako ya kila siku.

Tofauti ya Style Na Fashion

3) Je ni kweli umekipenda?

Kama tulivyosema mwanzo miluzi mingi humpoteza mbwa, inawezekana hata hio trend hujaipenda ni vile tu kila unapopita unakutana nayo mwishoe unaamua tu na wewe uwe nacho na matokeo yake kuishia kukaa kabati bila kuvaliwa

4) Je Utakivaa Hata Baada Ya Trend Kuisha?

Some trend zipo timeless zinaweza kuvalika hata baada ya ile hype kuisha na kuna nyingine ni za muda tu. Ambapo ikiisha muda wake ukija kuvaa unaonekana wa zamani unachoyakiwa kufanya ni kununua zile ambazo unaona hata mara baada ya trend kuisha unaweza kuzitumia tena

Well ni matumaini yetu tumeweza kukusaidia kwa namna moja au nyingine tuambie ni trend gani uliirukia na sasa huwezi kuvaa tena?

Related posts

3 Comments

  1. sig sauer for sale

    … [Trackback]

    […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/mitindo/maswali-ya-kujiuliza-kabla-hujanunua-kitu-kinacho-trend/ […]

  2. Buy Remington gun

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/maswali-ya-kujiuliza-kabla-hujanunua-kitu-kinacho-trend/ […]

  3. Mushroom Golden Teacher

    … [Trackback]

    […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/mitindo/maswali-ya-kujiuliza-kabla-hujanunua-kitu-kinacho-trend/ […]

Comments are closed.