SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mavazi Ya Kuepuka Endapo Una Mwili / Kimo Kidogo
Mitindo

Mavazi Ya Kuepuka Endapo Una Mwili / Kimo Kidogo 

Kupata mavazi ambayo yanaendana na kimo chako inaweza kuwa ni tatizo ambalo unakutana nalo mara kwa mara endapo wewe ni mfupi, yes hii inakuwa kama zamani ambapo watu wanene walikuwa wakikosa mavazi kutokana na makampuni kutumia sana vipimo vya models wembamba same na kwa wafupi makampuni mengi hutumia vipimo vya models warefu, ukipata mavazi basi lazima upeleke kwa fundi yapunguzwe.

Well leo tunaongelea vitu vya kuepuka endapo una mwili mdogo (mfupi)

  • Oversized Clothing

Tayari una mwili mdogo usiufunike zaidi kwa kuvaa mavazi makubwa, yes ni shida kupata mavazi yanayo tutosha lakini mafundi wapo hakikisha fundi ni rafiki yako, vaa mavazi yanayokutosha vyema na kama utavaa moja oversized basi lingine liwe perfect fit usivae juu na chini kote oversize.

  • Low Rise Jeans

Wengi tunapendelea kuvaa hizi ukizingatia wengi wenye maumbo haya huwaga hawana matumbo inakuwa perfect way ya kushow off, lakini tunasahau kwamba hizi suruali zinafanya kuonekena mfupi zaidi, badala yake vaa higwaist ambayo itakufanya miguu yako ionekane mirufu kuliko ambavyo ipo.

  • Chunky Shoes

Inawezekana katika fikra unawaza hivi viatu vinasaidia kuleta urefu lakini kiukweli hivi vinakumeza na vinatoa attention yote kwako na kupeleka miguuni, na vinafanya uzidi kuonekana mdogomdogo badala yake chagua viatu ambavyo simple havina mambo mengi kama converse, oxfords au kama ni mpenzi wa heels basi vaa heels zisikukuwa chunky au platfoarm.

  • Oversized Handbag

Oversized handbags ni sawa na chunky shoes, zinakumeza unazidi kuonekana mdogo badala yake chagua medium size ambazo zinaendana na mwili wako na kufanya attention isiondoke kwako.

Pictures By Naomi Bowyer

Related posts