SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mavazi Yako Ya Kulalia Yanavyo Athiri Usingizi Wako
Mitindo

Mavazi Yako Ya Kulalia Yanavyo Athiri Usingizi Wako 

Kuvaa mavazi / nguo ambazo zinaachia wakati wa usiku ni muhimu hasa katika mzunguko wa damu lakini pia kuifanya ngozi ipumue, kuvaa mavazi yanayo bana kama tight, mavazi yenye elastic kiunoni au tops za kubana zinaathiri mzunguko wako wa damu na kutatiza uwezo wako wa kupumua kawaida, na kunaweza pia kusababisha muwasho wa ngozi.

Vitu gani unatakiwa kufanya?

  • Usivae Brazia

Kuna uvumi wa kwamba unapolala na brazia basi inazuia maziwa kulala siku zijazo, lakini huu uvumi ni potofu, unapo lala ukiwa umevali brazia unaweza kujisababishia matatizo mbalimbali ikiwepo kuzuia mzunguko wa damu, kusababisha matatizo ya kutokupumua vyema lakini pia unaweza kupata fangasi hasa kwa wale tunaoishi maeneo yenye joto, na hii inatokea pia kwa wale ambao tunaopenda kulala na nguo za chini za kubana.

  • Vaa Mavazi / Nguo Zisizo Bana

Utafiti unaonyesha kuwa kuvaa nguo za kubana usiku kunaweza pia kuzuia utengenezaji wa melatonin ambayo inawajibika kudhibiti mzunguko wako wa usingizi, na ikiwa circadian rhythm mwili wako hauko sawa, basi hii inaweza kuathiri ubora wa usingizi wako.

  • Vaa Mavazi Ya Cotton (Pamba)

Pamba ndio material bora kabisa ya kulalia, inafaa kwa sababu ni nyuzi asilia ambayo ni nyepesi, laini na comfortable, zaidi ya hayo, inaruhusu ngozi yako kupumua na kuna uwezekano mdogo sana wa kusababisha mwasho wa ngozi au vipele, haswa ikiwa nguo haikubani Ikiwa pamba sio kwako, basi vitambaa vingine kama vile hariri au kitambaa cha mianzi (bamboo fabric) ni mbadala mzuri.

Well tuambie huwa unalala na mavazi ya aina gani?



																			

Related posts